Home Kimataifa Umewaona Paul na Florentin Pogba, hawa ni ndugu wengine kwenye soka.

Umewaona Paul na Florentin Pogba, hawa ni ndugu wengine kwenye soka.

8385
0
SHARE
Paul na Florentin Pogba hawa wamekuwa maarufu sana wiki hizi za karibuni.Umaarufu wao umeongezeka baada ya timu zao kupangwa pamoja katika hatua hii ya Europa League.Florentin ni mkubwa kwa Paul kwani Mathew ana miaka 26 na tofauti na Paul Pogba,Florentin Pogba yeye amezaliwa nchini Guinea.Lakini Paul na Mathias pia wana ndugu yao aitwaye Mathias ambae anachezea Sparta Rotterdam ya Uholanzi kwa sasa.Lakini hawa wafuatao pia ni ndugu.
LUIS SUAREZ NA PAULO SUAREZ.
Luis Suarez maisha yake ya soka na ukorofi wake aliiga kwa kaka yake.Kaka yake Luis aitwaye Paulo ndio chanzo cha Luis Suarez kupenda mpira.Tofauti kati ya Luis na Paolo ni kwamba Paolo yeye amecheza zaidi katika ligi za Marekani ya Kusini na kwa sasa yupo El Salvador,Paolo ana mika 36.
GILIANO NA GEORGENIO WIJNALDUM.
Geornenio ni maarufu zaidi kwa sasa,Georgenio ni kiungo muhimu Liverpool.Sio tu muhimu lakini Georgenio amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Liverpool akifunga goli muhimu dhidi ya vinara wa ligi Chelsea.Giliano yeye amekuwa akiichezea timu ya vijana ya Uholanzi lakini kwa sasa amepat bahati baada ya kusajiliwa ligi ya Marekani kwenye timu ya Philidephia Union.
TONI NA FELIX KROOS.
Mshindi wa kombe la dunia akiwa na Ujerumani na vile vile kiungo muhimu wa Real Madrid Toni Kroos.Toni Kroos huko Ujerumani amemuacha mdogo wake ambae nae anacheza soka na pia ni maarufu nchini humo aitwaye Felix Kroos.Felix anacheza katika timu inayoshiriki daraja la pili nchini humo iitwayo Union Berlin lakini kama kaka yake Felix naye ana ndoto za kuichezea Bayern Munich.
RODNEY NA WESLEY SNEIJDER.
Baba yao mzazi mzee Sneijdet inaonekana kama alipenda kuwapa wanae majina ya Kiingereza.Rodney ni kaka yake Wesley lakini yeye hakufanikiwa kucheza sana mpira kutokana na masula ya afya yake huku mdogo wake Wesley Sneijder akifanikiwa kucheza katika ligi kubwa barani Ulaya ikiwemo ligi ya Serie A.
TOBIAS NA BASTIAN SCHWEINSTEIGER.
Kiungo anayesugulia benchi Man United Bastian Schweinsteiger ana kaka yake aitwaye Tobias na yeye anapiga soka.Lakini wakati Bastian yeye akibeba makombe makubwa kubwa ikiwemo UEFA na kombe la dunia kwa Tobias yeye hali ni tofauti kwani alishindwa kucheza hata ligi kuu ya Ujerumani na kuishia ligi za chini na mwaka 1015 alistaafu.Kwa sasa Tobias ni kocha msaidizi wa timu ya vijana ya Ujerumani chini ya miaka 17.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here