Home Kimataifa Hapa kweli club hizi zilikula hasara ya pesa ndefu

Hapa kweli club hizi zilikula hasara ya pesa ndefu

9147
0
SHARE

Sio mara zote Ulaya wakifanua usajili unakuwa sahihi.Siku moja Pep Gurdiola alisema kitu kuhusu mshambuliaji wake mpta Gabriel Jesus Gurdiola alisema kumnunua Jesus ilikuwa kama tikiti maji hakuwa na uhakika na utamu wake hadi alipoliona ndani.Leo tujaribu kuona matikiti ambayo ndani ni mabaya,hii ni orodha ya baadhi ya sajili mbovu Uingereza.

1.Robinho.

Alisajiliwa kutoka Real Madrid kuja Man City na mbwembwe zikiwa nyingi sana huku yakitarajiwa makubwa kutoka kwa Mbarazil huyu.£32.5m zilimpeleka Robinho Etihad ikiaminika atafanya makubwa,mambo yalikuwa tofauti na ilivyotarajiwa kwake.Alipofunga goli la faulu dhidi ya Chelsea watu walianza kuona ubora wake lakini majeraha yalianza kumuandama.Man City waliamua kumpeleka kwa mkopo Santos huko akafunga magolin11 lakini aliporudi City hakufunga tena na City waliamua kumuuza Ac Millan kwa ada ya £15m.

2.Andriy Sheivchenko.
Huwezi hata kidogo kumuacha Sheivchenko ukitaja orodha ya saini mbovu kuwahi kusainiwa Chelsea.Mourinho alimleta Sheivchenko Chelsea kwa ada ya £30m lakini akaboronga sana huku Didier Drogba akichukua ufalme wa Chelsea kwa kipindi hicho na utawala wa Drogba uliwafanya Chelsea wazidi kuona kwamba walikula hasara kwa Sheivchenko.
3.Fernando Torres.
Baada ya kung’ara sana akiwa na Liverpool haikuwa shida kwa tajiri wa Kirussi Roman Abromovich kuingia mfukoni na kutoa £50m kumsajili Torres toka Liverpool.Kilichokuja tokea baada ya Torres kununuliwa ni hadithi ambayo mashabiki wa Chelsea duniani kote hawapendi kuisikia.
4.Juan Sebastian Veron.
Heshima ya Alex Ferguson ilitikisika hapa baada ya kufanya usajili mbovu.Veron hakuwa mbovu tu ndani ya uwanja alishindwa kuimarika ndani na nje ya uwanja huku akikwaruzana mara kadhaa na Sir Alex.Veron alishindwa kabisa kuendana na soka la Uingereza toka asajikiwe kwa ada ya £28m toka Lazio.Baada ya United kushindwana nae walumuuza kwa ada ya hasara ya £15m kwenda Chelsea.
5.Robbie Keane.
Wakati Benitez akiwa na Torres Liverpool,alihitaji mshambuliaji wa kusaidiana nae.Benitez alimuona Robbie Keana toka Tottenham kama mtu sahihu wa jambo hilo.Liverpool walipomsajili Robbie Keane alicheza mechi 27 huku akiwa amefunga magoli 7 tu na Liverpool kuamua kumrudisha Totenham.
6.Sergei Rebrov.
Mshambuliaji kutoka Ukraine ambae alikuja Uingereza kumfuata Mukraine mwenzie Andrie Sheivchenko.Japokwa hawakuwa timy moja kwani Rebrov yeye alienda Totenham kwa ada ya £11m kutoka Dynamo Kiev.Katika mechi 85 alizoichezea Totenham Rebrov alifunga magoli 15 tu akiajwa kama mchezaji mbovu kuwahi kununuliwa Totenham.
7.Andy Caroll.
Kwa mashabiki haswa vijana ukiwauliza kuhusu sajili mbovu kuwahi kufanywa Liverpool usajili huu hauwezi kukosa.Baada ya kuwa na msimu mzuri sana na Newcastle United,Liverpool walivunja kibubu na kutoa £35m kumnunua Caroll.Caroll alivurunda mno Liverpool na majeraha yalichangia.Liverpool waliamua kumuuza Caroll kwenda West Ham kwa adaya £17m.
8.Steve Marlet.
Fulham ilikuwa kati ya klabu za kuogopwa Uingereza.Fulham ili kuimalisha klabu yao waliipa Lyon £11m kumnunua Steve Marlet.Sio tu kiwango kibovu lakini Marlet alikuwa chanzo cha suala la rushwa kati ya kocha wa Fulham Jean Tigana na timu hiyo,baadaye mwenyekiti wa Fulham alimuuza Marlet na kuachana na Tigana.
9.Memphis Depay.
Uholanzi aliitwa Ronaldo Mpya,uwezo wake wa uwanjani ulionesha kweli huenda akawa Ronaldo mpya.Manchester United walupomnunua toka PSV Eindhoven walitaraji atakuwa Ronaldo mpya kweli na kumpa jezi namba 7.Lakini akiwa United aliishia kununua magari ya kifahari na kuweka mitindi mipya ya nywele,Mourinho hakumvumilia alimuuza kwenda Olympique Marsseile.
10.Cristian Benteke.
Akiwa Aston Villa alionekana tishio sana,vigogo wengi walimmezea mate lakini aliishia kwenda kukipiga Anfield.Katika mechi 42 chini ya Kenny Danglish alifunga magolu 10 tu.Ni kama vile Liverpool walikuwa na bahati kwani walimuuza Benteke kwenda Crystal Palace kwa hela kubwa kidogo,walimuuza kwa £27m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here