Home Kimataifa Watu 17 wafariki uwanjani Angola, ni funzo kwetu.

Watu 17 wafariki uwanjani Angola, ni funzo kwetu.

2944
0
SHARE

Inakadiriwa watu wapatao 17 wamefariki huko nchini Angola Ijumaa iliyopita wakati wa mchezo kati ya Santa Rita De Casia dhidi ya Reactrativo De Libolo.Polisi wanasema katika miili iliyokutwa uwanjani hapo baada ya tukio hilo kulikuwa na wanawake na watoto huku kukiwa na majeruhi zaidi ya 56 katika tukio hilo.Mechi hiyo inasemekana washabiki wengi hawakuwa na tiketi na hivyo uwanja kufurika kupita kawaida.

Tukio la Angola linakuja ikiwa imepita miaka16 tangu tukio lililopoteza maisha ya mashabiki wengi kutoke Africa.Hii ilikuwa mwaka 2001 mjini Accra Ghana.Ilikuwa katika uwanja wa Accra Sports Stadium ambako kulikuwa na mpambano wa miamba wawili wa nchini humo timu ya Accra Hearts of Oak dhidi ya timu ya Asante Kotoko.Katika mchezo huu takribani mashabiki 127 walifariki katika tukio hilo.
Miaka 9 baada ya tukio la Ghana,tukio lingine lilitokea nchini Ivory Coast katika mchezo wa kufudhu kombe la dunia uliopigwa Stade Felix Houfuete kati ya wenyeji Ivory Coast dhidi ya Malawi na katika tukio hili mashabiki 19 walifariki dunia.
Miaka 16 iliyopita nchini Afrika Kusini kwenye Sowetho Derby kati ya Kaizer Chiefs na Orlando Pirates mashabiki 43 walifariki dunia.Hii ilitokana na mashabiki kujazana kupitiliza idadi kamili inayotakiwa kuingia,inasemekana mashabiki 30,000 walizidi kwenye mchezo huo.
Matukio mengi ya majanga haya katika ukanda huu wa Afrika huwa yanatokana na uzembe wa mashabiki wenyewe,vyombo vya usalama au vyama vya soka.Suala la ticket feki ndio limeua watu Angola jambo ambalo hapa kwetu tiketi feki ni nyingi sana hasa katika mchezo wa Dar Derby.
Waswahili wana msemo wao ya kwamba ukiona mwenzio ananyolewa anza kutia maji kichwa chako.Tumeshawai kuona mara nyingi mageti ya uwanja wa taifa yakivunjwa (Yanga vs Tp Mazembe) nivyema kuanza kuchukua hatua mapema kabla tukio kama hili halijatokea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here