Home Kimataifa United wangekula hasara ya £100M kwa Muller.

United wangekula hasara ya £100M kwa Muller.

2856
0
SHARE

Thomas Muller msimu uliopita alikaribia kutua katika ligi ya Uingereza kwa ada kubwa sana ya usajili.Muller alihusishwa kutua Manchester United kwa £100m ada ambayo United wangewapa Bayern Munich kama wangefanikiwa kupata sahihi ya Muller.

Inaonekana sasa United wanashukuru kutokumchukua Muller kwani wangekula hasara.Kiwango cha Thomas Muller msimu huu sio kama kile cha msimu uliopita,Muller huyu wa sasa sio Muller wa mwaka jana,Muller aliyekuwa chini ya Gurdiola na Muller wa chini ya Ancelotti wamefanana sura lakini viwango vikiwa tofauti kabisa.
Msimu uliopita Thomas Muller alikuwa katinya washambuliaji hatari sana katika kuzifumani nyavu lakini msimu huu mambo yamekuwa tofauti sana.Muller amefunga goli moja tu katika michezo 19 ya ligi msimu huu huku akitoa assist 5 tu hali ambayo sio nzuri sii tu kwa Muller bali pia kwa Bayern Munich.Muller amekuwa akilalamika kwa kusema kwamba ni ngumu yeye kucheza vizuri kama timu haiko vizuri.
Toka alipokosa penati katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Athletico Madrid msimu uliopita Muller amekuwa mbovu.Penati hiyo ilimfanya Muller kuwa Mjerumani wa pili kukosa tuta katika hatua za mtoano kwenye michezo ya kimataifa huku wa kwanza akiwa Ulli Stielike aliyekosa penati kwenye kombe la dunia mwaka 1982.
Muller msimu huu alicheza dakika 999 bila kufunga goli hata moja lakini baadae alipata goli dhidi ya Wolfburg.Haijaeleweka endapo Ancelotti atatafta mshambuliaji mwingine katika dirisha lijalo lakini pia Muller hana dalili za kuondoka Bayern na anaonekana kufurahia tu maisha ya Ujerumani.
Muller mwenye umri wa miaka 27 ni mtihani kwa Bayern Munich kwani yeye ni kati ya wachezaji wakutumainiwa wenye umri chini ya miaka 30 klabuni hapo.Hivi sasa wachezaji muhimu “key players” watano wa Bayern Munich wameshavuka miaka 30 na inaonekana hawana uhakika kukaa kwa muda mrefu klabuni hapo akiwemo Arjen Roben na kapteni Phillip Lahm ambae inasemekana anakaribia kustaafu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here