Home Kimataifa Mmemkera Clattenburg, Huyoo Anaiacha EPL Anaenda Zake Saudi Arabia.

Mmemkera Clattenburg, Huyoo Anaiacha EPL Anaenda Zake Saudi Arabia.

3511
0
SHARE

Inaoenekana safari imekwiva na sasa refarii, Mark Clattenburg ataondoka kwenye ligi kuu ya Uingereza na ataelekea zake nchini Saudi Arabia.

Ripoti zilizotoka wiki hii zinasema mwamuzi huyo ambaye ndiye anayehesabiwa kuwa bora zaidi kwa sasa nchini humo, alipata ofa kutoka katika nchi tofauti lakini inaonekana ameamua kuelekea mashariki ya Kati.

Inasemekana kuwa Clattenburg ameendelea kuchoshwa na kiwango cha kukosolewa na uchunguzi uliopitiliza ambao huyokana mara nyingi na michezo mikubwa mfano ukiwa goli la mkono la Alexis Sanchez kwenye ushindi wa mabao 2-0 wa Arsenal dhidi ya Hull City.

Mark Clattenburg will leave the Premier League and move to Saudi Arabia

Chama cha waamuzi kimethibisha kuwa Clattenburg amefikia maamuzi hayo siku ya leo Alhamis, na kimetoa taarifa ya kumtakia kila lakheri kwenye maisha yake mapya.

‘Chama cha marefarii (PGMOL) kingependa kumtakia kila jema Mark Clattenburg wakati huu anapoelekea nchini Saudi Arabia kuungana na shirikisho la soka nchini humo Saudi Arabian Football Federation,’ waliandika.

‘Tangu ajiunge na PGMOL mwaka¬† 2004, Mark alipanda viwango mpaka kuwa mmoja wa waamuzi bora, akihusika na kusimamia michezo mikubwa duniani huku akiwa mfano wa wengine kufuata nyayo. Mafanikio yake yalielekea mpaka msimu uliopita ambapo Mark alikuwa mwamuzi kwenye michezo ya fainali Kombe la FA,¬† Fainali ya ligi ya Mabingwa na fainali ya UEFA Euro mwaka 2016.

He is said to have become frustrated at the scrutiny referees come under in English football

Clattenburg alikiri mwaka jana mwezi Desemba kuwa kwenda kuchezesha michezo nchi nyingine lilikuwa jambo analolifikiria.

‘Kama nafasi ikija tutatizama uwezekano, nina mkataba na ligi kuu ya Uingereza lakini pia lazima nitizame mipango yangu ya muda mrefu kwa maisha yangu. Nitadumu kwa muda nikiwa mwamuzi?

‘Hakuna ofa iliyofika mezani lakini kama kuna ofa nzuri ikifika basi nitaitizama mara mbili na kuifikiria alisema kipindi hicho’

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here