Home Kitaifa Hatimaye Manji ameachiwa kwa dhamana baada ya kukaa sero kwa siku 7

Hatimaye Manji ameachiwa kwa dhamana baada ya kukaa sero kwa siku 7

8577
0
SHARE

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji, leo February 16 amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la kutumia dawa za kulevya kinyume na sheria.

Inadaiwa mnamo tarehe 06/02/ 2017 na 09/02/2017, Manji alitumia dawa za kulevya aina ya Heroine kinyume na sheria ambapo Manji amekana shitaka alilosomewa.

Mawakili wanaomtetea Manji wakiongozwa na Alex Mgongolwa waliiomba mahakama kumwachia mteja wao kwa dhamana.

kwa upande wa mawakili wa mashtaka, hawakuwa na pingamizi na dhamana licha ya upelelezi wa shauri hilo kutokamilika.

Mahakama ilikubali ombi la dhamana yenye masharti ya mdhamini mmoja mwamwinifu na kiasi cha shilingi za Tanzania milioni 10.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa akajitokeza kumdhamini Manji. Baada ya kukamilika kwa taratibu zote za dhamana, Manji akaachiwa na kesi yake kutajwa kusikilizwa tena March 16, 2017.

Manji aliwekwa mahabusu tangu February 9, 2017 aliporipoti kwenye kituo kikuu cha Polisi Dar (Central) akituhumiwa kujihusisha kwa dawa za kulevya kabla ya kuachiwa leo kwa dhamana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here