Home Kitaifa George  Kavila: Mexime anairudisha Kagera Sugar, tutaendelea kufunga magoli…

George  Kavila: Mexime anairudisha Kagera Sugar, tutaendelea kufunga magoli…

2571
0
SHARE
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa pambano la fainali kati Mtibwa Sugar vs URA FC

Na Baraka Mbolembole

KAMA watafanikiwa kuifunga Tanzania Prisons katika mchezo wa jioni ya Leo katika uwanja wa Sokoine, Mbeya, timu  ya Kagera Sugar FC itarejea katika nafasi ya Tatu ya msimamo  huku wakifikisha pointi 40 ambazo zitawafanya kuwa nyuma ya alama 11 nyuma ya vinara Simba SC na alama Tisa nyuma ya mabingwa watetezi Yanga SC.

Kagera ilinusurika kushuka daraja msimu uliopita lakini tangu kuwasili kwa kocha kijana Mecky Mexime katika timu hiyo ya Bukoba, Kagera mambo yamekuwa yakienda vizuri.

Mecky aliwasaini wachezaji wazoefu kama Danny Mrwanda, golikipa Juma Kaseja na wachezaji vijana kama Edward Christopher, Mbaraka Yusuph na Ibrahim Twaha ‘Messi’ na hadi sasa kikosi chake kikiwa kimecheza michezo 21 kimefanikiwa kushinda michezo 11, mechi 6 wamepoteza na nyingine nne wametoa sare.

“Malengo yetu ni kumaliza ligi katika nafasi tatu za juu.” Anasema nahodha wa kikosi hicho kiungo, George Kavila nilipofanya naye mahojiano akiwa Mkoani Mbeya ambako watacheza na Prisons Leo Jumatano.

“Mechi ya leo ni ngumu ila yote kwa yote tutajitahidi kushinda. Uwezo wa kushinda tunao.” Anasema mchezaji huyo  wa muda mrefu kikosi Kagera.

“Kwa sasa tuna kikosi kizuri chenye mchanganyiko wa wachezaji vijana na wale wazoefu

Kitu kizuri ni kwamba vijana wamekuwa na nidhamu ya hali ya juu, wanapenda kujifunza na heshima katika timu ipo kwa kiwango cha juu huku upendo miongoni mwa wachezaji ukichochea timu kuendelea kufanya vizuri.

Kagera ilifungwa 6-2 na Yanga katika mchezo wa raundi ya kwanza kasha wakapoteza tena mbele ya Azam FC hali iliyofanya baadhi ya mashabiki wa soka mkoani Kagera kuhoji uwezo wa kocha Mecky.

“Tulipoteza mechi ile ya Yanga kwa sababu ya uchovu tu hakuna kingine pia tukapoteza mchezo uliofuata  dhidi  ya Azam, lakini kocha Mecky alituambia ni matokeo tu ya mchezo na hatupaswi kukata tama. Alitujenga vizuri kisaikolojia  na mpaka sasa  umeshasahau na tunaangalia mbele.

“Ukitazama kikosi chetu jinsi kinavyocheza msimu huu utagundua ni kiasi gani kocha Mecky amefanikiwa kuibadilisha timu iliyokuwa dhaifu na kuifanya iwe bora. Kagera hii ya sasa naifananisha na ile ya misimu miwili iliyopita, tunacheza vizuri na tunaweza kushinda katika uwanja wowote-nyumbani au ugenini.” Anasema Kavila

Kagera  imefanikiwa  kufunga magoli  24  na  kuruhusu  nyavu  zao  mara  20  katika  michezo  21  waliyokwishacheza  katika  ligi. Ili  waendelee  kuwa  bora  wanapaswa kuongeza nguvu  katika  mashambulizi  na kuongeza  mfungaji  wa nyongeza  na   kuacha  kumtegemea  Mbaraka  Yusuph  pekee  ambaye  tayari  amefunga magoli   9.

“Mwalimu  ndiye  anajua nini cha kufanya ili timu ifunge magoli na kuzuia vizuri. Muda mwingi amekuwa akiwaelekeza mabeki nini cha kufanya, lakini mpira ni mchezo wa makosa na ili ufungwe unatakiwa kufanya makosa. Tunajitahidi sana kurekebisha makosa yetu, na kuhusu kufunga magoli zaidi hilo sina shaka nalo. Tutafunga kwa sababu wafungaji wapo.”

Februari24 timu hiyoitacheza na Stand United ya Shinyanga katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa michuano ya FA Cup.

“Itakuwa mechi ngumu, tunawaheshimu Stand ni timunzuri ila sisi ni wazuri zaidi yao na tumedhamilia kufanya vizuri katika michuano hiyo pia ikiwezekana kushinda ubingwa  ili  tuiwakilishe nchi katika michuano ya Afrika mwaka ujao.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here