Home Kitaifa Offer za Ulaya zilizowahi kumfikia Himid…kwa nini bado yupo Azam?

Offer za Ulaya zilizowahi kumfikia Himid…kwa nini bado yupo Azam?

9535
0
SHARE

Hakuna mtu asiyependa mafanikio katika kazi anayoifanya, mafanikio kwa upande wa wachezaji wa kibongo ni kupata fursa ya kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania hususan bara la Ulaya.

Watu wengi wamekuwa wakiwapigia kelele wachezaji wa Tanzania kupambana kuhakikisha wanapata nafasi hizo wakiamini huko wataongeza uzoefu, wataimarisha viwango vyao pamoja na weledi lakini pia hata vipato vyao vitaongezeka.

Nilipopata fursa ya kuzungumza na Himid Mao Ninja au ‘Engine ya Boat’ sikuacha kumuuliza kama ana mpango wa kutoka Tanzania kwenda nje kucheza soka nikiamini anaweza kutokana na uwezo wake mkubwa anaounesha akiwa uwanjani kila anapoitumikia klabu yake ya Azam pamoja na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars.

“Zimewahi kuja offer mbili, moja ilikuwa inatoka Slovenia na nyingine ilikuwa inatoka Denmark sijui nini kilitokea lakini mwisho wa siku hawakufikia makubaliano wao wan a Azam ila kwa upande wangu nilikuwa niko tayari,” – Himid Mao

“Nilishaanza hadi michakato ya visa kwa ajili ya hilo deal la Denmark na tulishalipa kila kitu lakini mwisho wa siku haikutoka ruhusa kutoka Azam. Kipindi hicho tulikuwa kwenye mashindano ya Confederation tunacheza mechi na Esparance kwa hiyo  haikuwa rahisi kwa Azam kuniachia kwa kipindi hicho.”

“Hakuna mtu asiyependa kucheza kwenye mazingira bora zaidi, lakini issue ni kwamba mimi nipo kwenye mkataba kwa hiyo wao ndiyo wanashikilia haki yangu mimi, wakisema nenda naenda, wakisema huwezi kwenda siwezi kulazimisha kwa sababu wao ndio waajiri wangu wa sasa lakini ningekuwa huru ningekuwa naamua kile nachotaka.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here