Home Kitaifa Taratibu zimefatwa Nyenzi na wenzake kurudishwa Yanga?

Taratibu zimefatwa Nyenzi na wenzake kurudishwa Yanga?

5889
0
SHARE
Mwanacha na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Ayubu Nyezi (wa kwanza kulia) yeye na wenzake wawili wamerejeshwa ndani ya klabu ya Yanga baada ya awali kuvuliwa unachama

Baada ya klabu ya Yanga kupitia katibu wake mkuu Charles Boniface Mkwasa kuiandikia barua TFF kuijulisha kwamba, mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji amewasamehe na kuwarejeshea uanachama na nyadhifa zao wanachama watatu waliokuwa wamevuliwa uanachama, kitendo hicho kimeonekana kimekwenda kinyume na taratibu.

Ikumbukwe wanachama hao (Ayub Nyenzi, Salum Mkemi na Hashim Abdallah) ambao walivuliwa uanachama na mkutano mkuu, swali linaloibuka ni kwamba, kwa nini uanachama wao warejeshewe kwa barua pasipo mkutano mkuu kujadili na kuona inafaa kuwarejeshea uanachama wao?

Wakili wa kujitegemea Philip Rungu amesikika kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM akifafanua uhalali wa wanachama hao kurejeshwa kwenye timu kwa barua ya kiofisi pekee.

“Kama mamlaka ya kumfukuza ni yamewekwa ndani ya mkutano mkuu au baraza, basin a mamlaka ya kurejesha yanakuwa hivyohivyo kwa mkutano mkuu,” – Rungu.

“Nadhani barua inaonesha kwamba, mwenyekiti amesamehe wale watu watatu sasa swali linakuja, je mwenyekiti ndio anayehitimisha kolamu ya mkutano mkuu? Nadhani jibu lake ni hapana, sasa mamlaka ya kuwarejesha ni mkutano mkuu wa klabu.”

“Labda wangepeleka ripoti kupitia kwa katibu mkuu kueleza kwamba, kutokana na sababu kadhaatunaomba mkutano mkuu uweze kuridhia kwamba watu hawa waweze kusamehewa halafu mkutano mkuu unaazimia azimio la kwamba watu hao wasamehewe na warejeshwe kwenye klabu na uanachama wao unakuwa hai, nadhani kiutaratibu watakuwa wamekosea.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here