Home Kitaifa Mpango wa TFF kuwanusuru Serengeti Boys na utumiaji wa dawa za kulevya

Mpango wa TFF kuwanusuru Serengeti Boys na utumiaji wa dawa za kulevya

1452
0
SHARE

Madawa ya kulevya ndio habari kubwa sasa, kutokana na athari za madawa hayo kwa vijana ambao ndio nguzo ya nchi, Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF limeandaa ziara ya mafunzo kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ili kuwaepusha na janga hilo.

Serengeti itapelekwa Bagamoyo Machi 4 kutembelea kituo cha waathirika wa dawa za kulevya kiitwacho ‘Life and Hope Rehabilitation Center’ kwa ajili ya kujifunza kwa kuona madhara yatokanayo na matumizi ya madawa hayo.

Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas alisema vijana hao wameanza kukua na kuwa na mabadiliko mbalimbali ya miili yao na ndio kipindi ambacho wanataka kujaribu kila kitu hali ambayo isipochukuliwa kwa umakini inaweza kuleta madhara makubwa.

Lucas alisema kuwa katika ziara hiyo watapeleka zawadi mbalimbali kwa waathirika hao ili nao wajione ni sehemu ya jamii na kuonyesha kuwa wameguswa na janga hilo pamoja na kushiriki katika jitihada za Serikali za kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya.

“Vijana wa Serengeti nao wanakua sasa, wanatamani kujaribu vitu vingi, wanataka kuwa na wapenzi kufanya mambo mbalimbali kwa kuwa wanajiona ni wakubwa kwahiyo tutawapeleka Bagamoyo ili wakajionee madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya,” – Alfred Lucas.

Katika ziara hiyo TFF itatoa usafiri kwa waandishi wa Habari kwa ajili ya kwenda kuripoti tukio hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here