Home Kitaifa Achana na mbio za Simba na Yanga katika taji, ‘vita ya kuvutia’...

Achana na mbio za Simba na Yanga katika taji, ‘vita ya kuvutia’ inazihusu timu hizi Tano…

7032
0
SHARE

Na Baraka Mbolembole

JKT Ruvu ilifanikiwa kupata ushindi wa kwanza katika ligi kuu Tanzania Bara tangu  Oktoba 29, 2016 walipoifunga Ndanda FC 1-0.

Ushindi wao wa tatu  katika ligi msimu huu umepatikana siku ya Jumapili baada ya kuifunga Mbao FC 2-0 katika uwanja wa Mkwakwani,Tanga ambao kikosi hicho cha kocha Bakari Shime kimehamia katika uwanja huo baada ya kushindwa kupata matokeokatika uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.

Ushindi huo umewafanya kufikisha alama 19 na ‘kufufua’ upya mkakati wao wa kuondoka mkiani ambako wameganda tangu mwanzoni mwa msimu  huu. Wakati JKT Ruvu ikipata ushindi huo timu nyingine nne zilizo katika harakati za kukwepa ‘mkasi’ wa kushuka daraja zilishindwa kupata matokeo.

Ndanda FC  walio nafasi ya 15 walishindwa kupata ushindi wakicheza nyumbani, Nangwanda  baada ya kulazimishwa suluhu-tasa na Toto Africans ya Mwanza. Suluhu hiyo imewafanya Ndanda kufikisha alama 20 baada ya kucheza michezo 22 (pointi moja zaidi ya JKT Ruvu inayoburuza mkia).

Mchezo huu ulikuwa muhimu kwa kila timu na inawezekana pointi moja waliyopata Mtwara ikawa namaana kubwa kwa Toto kwani wameisimamisha timu ambayo ingewafunga ingewasukuma chini ya msimamo .Toto wamebaki nafasi 13 wakiwa na alama 21 sawa na Majimaji FC.

Majimaji FC walionafasi ya 14-ambayo ni nafasi ya mwisho kwa timu tatu zitakazoshuka daraja ilipata pointi moja muhimu ugenini dhidi ya Stand United siku ya Jumamosi baada ya kulazimisha suluhu (0-0) ambayo imewafanya kufikisha pointi 21 baada ya kucheza michezo 22.

Ikicheza nyumbani siku ya jana Jumapili, timu ya African Lyon ya Dar es Salaam ilikubali sare ya kufungana 2-2 na Mtibwa Sugar na hivyo kufikisha alama 22 huku kiendelea kubaki katika nafasi ya 12.

Ni wastani wa pointi tatu tu kati yao ya timu ya mwisho katika msimamo hivyo kwa namna yoyote ile kikosi hicho bado kinatakiwa kufanya kazi kubwa katika michezo yake nane iliyosalia.

NANI ATASHUKA?

Zikiwa zimesalia mechi 8 kwa kila timu kati ya timu tano zilizo katika vita ya kuepuka kutoshuka daraja ni wazi VPL msimu huu itakuwa na ushindani mwingine mkubwa chini ya msimamo kuliko katika mbioza ubingwa ambako ni wazi Simba SC na mabingwa watetezi Yanga SC ndiyo watashinda hadi mwisho kuwania ubingwa huo.

JKT RUVU

JKT Ruvu imebakisha michezo 7 baada ya kucheza michezo 23 hadi sasa na kati ya michezo iliyosalia upande wao game tatu watacheza dhidi ya timuambazo pia zinapigana kutoshuka daraja.

Watacheza na Mtibwa Sugar (ugenini Turiani), Mwadui FC (ugenini Mwadui Complex), Kagera Sugar FC (ugenini Kaitaba, Bukoba), Azam FC (nyumbani Mkwakwani,Tanga), Ndanda FC  ( ugenini, Nangwanda, Mtwara), Majimaji FC (nyumbani Mkwakwani) na watamaliza msimu kwa kucheza na Toto Africans (ugenini, Kirumba, Mwanza).

Hakika ni ratiba ngumu sana kwao na baada ya kunusurika kushuka misimu mitatu mfululizo kikosi hicho ambacho hakijawahi kushuka daraja tangu mwaka 2002 walipopanda kwa mara ya kwanza watapaswa kukaza ’buti’ zao msimu huu ili wasishuke.

NDANDA FC

Timu hii ya Mtwara ilipanda ligi kuukwa mara ya kwanza msimu wa 2014/15 hakika wapo katika jaribio kubwa zaidi la kuhakikisha hawateremki daraja msimu huu, michezo yao nane ijayo itakuwa dhidi ya African Lyon (nyumbani) Ruvu Shooting (nyumbani), Mbao FC (nyumbani) kisha watasafiri kuelekea Mbeya kuchezana Mbeya City.

Wataivaa Mwadui FC (ugenini),  halafu watarejea nyumbani Nangwanda kuwakabili JKT Ruvu kisha waenda kumalizia ligi ugenini dhidi ya Tanzania Prisons na baadaye Stand United.

Kama wataitumia vizuri michezo mine ya nyumbani huku miwili wakicheza na timu  zinazopigana kutoshuka, Ndanda wanaweza kunusurika japokuwa haitakuwa michezo rahisi pia.

MAJIMAJI FC

Kikosi hiki cha kocha kijana Kally Ongala kilinusurika kushuka msimu uliopita na ili wasirejee ligi daraja la kwanza wanapaswa kufanya vizuri katika michezo yao nane iliyosalia. Watakutana na timu mbili zilizo katika harakati za kutoshuka daraja.

Majimaji watacheza na Mbao FC (ugenini, Kirumba, Mwanza), Kagera Sugar (ugenini, Kaitaba), kisha watarejea nyumbani Majimaji Stadium kucheza na Toto Africans na African Lyon.

Baada ya michezo hiyo watawavaa Ruvu Shooting (ugenini, Mlandizi, Pwani), watarejea nyumbani kuwavaa Mbeya City kisha wataenda Tanga kuwavaa JKT Ruvu halafu watamaliza msimu kwa kucheza nyumbani dhidi ya Mwadui FC.

TOTO AFRICANS 

Timu hii ya Mwanza imekuwa na kawaida ya kushuka na kupanda daraja na sasa wakiwa nafasi ya 13, Toto wanapaswa kufanya vizuri zaidi katika michezo yao nane iliyosalia ili wasishuke daraja baada ya kupanda misimu miwili iliyopita.

Michezo  yao nane iliyosalia ni dhidi ya Kagera Sugar, Mbao FC (mechi zote watacheza nyumbani Kirumba, Mwanza). Watacheza pia na Majimaji FC (ugenini,) Yanga SC (ugenini), Simba SC (nyumbani), Mtibwa Sugar (ugenini), Azam  FC (ugenini) kisha watamaliza msimu kwa kuwavaa JKT Ruvu nyumbani Kirumba Stadium.

Ratiba yao ni ngumu sana lakini hawana namna ya kufanya zaidi ya kuhakikisha wanakusanya walau alama 12 katika game nane zilizosalia upande wao.

AFRICAN LYON

Timu hii ilirejea VPL msimu huu lakini wana wakati mgumu katika ligi. Lyon ipo nafasi ya 12 lakini ni tofauti ya pointi tatu tu kati yake na JKT Ruvu inayoshika mkia, imechezamichezo 22 na kusaliwa na michezo nane.

Mechi zao zilizobaki katika ligi ni dhidi ya  Ndanda FC (ugenini), Mwadui FC (nyumbani), Stand United (nyumbani), Majimaji FC (ugenini),  Mbeya City FC (ugenini), Tanzania Prisons (ugenini), Ruvu Shooting (nyumbani), na watamaliza msimu kwa kuwavaa Simba SC.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here