Home Kitaifa Omog ameanza kutafuta dawa ya Yanga

Omog ameanza kutafuta dawa ya Yanga

4809
0
SHARE

Zainabu Rajabu.

KOCHA mkuu wa  Simba Joseph Omog amesema sasa  mipango yao ni kushinda kila mechi iliyo mbele yao huku  msimamo huo ukiungwa mkono na wachezaji  wake  kwa asilimia mia.

Simba ina mtihani mkubwa tarehe 25 dhidi ya wapinzani wao (Yanga) ambao wamewazidi alama mbili katika msimamo wa ligi, lakini Yanga wana mchezo mmoja wa kiporo uliotokana na Yanga kusafiri kwenda nje ya nchi kucheza mechi ya klabu bingwa Afrika.

Omog amesema amewasihi wachezaji wake kujituma na kupambana ili kila mchezo wanaocheza wuibuke na pointi tatu ili kuongeza wigo wa alama kwa wapinzani wao.

“Akili yangu inawaza jinsi gani nitawapa mbinu mpya na nzuri  wachezaji wangu za kuwamudu vizuri mastraika wa Yanga  ambao wamekuwa na uchu wa kufunga,” – Joseph Omog.

Kikosi cha Simba kimeingia leo kujiandaa na mchezo wao  wa kombe la shirikisho   dhidi ya African Lyon siku ya Alhamis katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here