Home Kitaifa Kijuso ameomba huruma ya waamuzi

Kijuso ameomba huruma ya waamuzi

2916
0
SHARE

Kocha msaidizi wa Mbeya City Mohamed Kijuso ameomba waamuzi wa ligi kuu Tanzania bara kuchezesha soka kwa usawa huku wakifata sheria zote za mchezo huo ili kila timu ipate haki yake.

Hayo yote ni kutokana na timu yake kupoteza mchezo mchezo wa ugenini kwa kipigo cha goli 3-2 kutoka kwa Mwadui FC ya Shinyanga.

“Naomba wamuzi kidogo wawe fair kwa sababu tunapokuja sehemu kama hizi, tunatumia gharama nyungi na wao watonee huruma na sisi ni binadamu vilevile,” – Mohamed Kijuso.

“Inabidi tupambane na vijana wangu ili kuweza kutoka na pointi Kanda ya Ziwa.”

Magoli ya Mwadui FC yalifungwa na Hassan Kabunda aliyefunga mara mbili na goli jingine likafungwa na Paul Nonga wakati magoli yote mawili ya Mbeya City yakifungwa na Raphael Daudi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here