Home Kitaifa AUDIO: ‘Mwamuzi angewaacha kidogo tu, tungepata ushindi’ – Stamili Mbonde

AUDIO: ‘Mwamuzi angewaacha kidogo tu, tungepata ushindi’ – Stamili Mbonde

3407
0
SHARE
Mshambujili wa Mtibwa Sugar Stamili Mbonde (kulia) akichuana vikali na beki wa kati wa African Lyon Hassan Isihaka kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa uwanja wa taifa February 12, 2017

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Stamili Mbonde amesema mechi yao dhidi ya African Lyon ilikuwa rahisi kwao lakini mwamuzi wa mchezo huo Mathew Akrama wa Mwanza aliwabeba wapinzani wao kitu kilichopelekea mchezo huo kumalizika kwa sare ya kufungana 2-2.

Mchezo huo ulikuwa ni wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru huku African Lyon wakiwa ndio wenyeji wa pambano hilo.

“Mchezo ulikuwa mzuri lakini sio kama ule tuliocheza nyuma, huu ulikuwa umepoa lakini mwamuzi alikuwa upende wao (African Lyon) kama mwamuzi angechezesha fair basi tungepata ushindi,” – Stamili Mbonde.

“Mchezo huu kwetu ulikuwa mwepesi kuliko wa nyuma ambao tulifungwa lakini mechi ilikuwa nzito sana ukilinganisha nah ii ambayo ilikuwa nyepesi sana, ila kama mwamuzi angewaachia kidogo tungepata ushindi.”

“Sisi wapambanaji sehemu yoyote tukiingia tunataka kushinda.”

Wachezaji wa Mtibwa Sugar magoli ya African Lyon ambayo yote yalitokana na mikwaju ya penati na kufungwa na beki wa kati wa timu hiyo Hassan Isihaka.

Kabla ya mchezo dhidi ya Lyon, Mtibwa ilipoteza mchezo wake wa ugenini mkoani Mwanza kwa kipigo kikubwa zaidi cha magoli 5-0 kutoka kwa Mbao FC.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here