Home Kitaifa Yanga yatoa kipigo kizito kwa Wacomoro

Yanga yatoa kipigo kizito kwa Wacomoro

5376
0
SHARE

Mabingwa wa Tanzania na wawakilishi wa nchi katika michuano ya klabu bingwa ya Afrika, Yanga, leo wameianza vyema kampeni yao ya kuuwania uchampion wa Afrika wakiwa ugenini nchini Comoro.


Wakicheza katika dimba la Stade De Moroni, Yanga wamefanikiwa kuifunga Ngaya Club magoli 1-5.

Alikuwa ni kiungo Justine Zullu aliyefungua ukurasa wa magoli katika dakika ya 43 ya mchezo, na sekunde kadhaa kabla ya filimbi ya mwisho Msuva Simon akafunga goli la pili.

Kipindi cha pili Yanga wakarejea kwa kasi ile ile na kuandika goli la 3 kupitia Chirwa katika dakika ya 59, kabla ya Ngaya kupata goli la kufutia machozi dakika 8 baadae lilofungwa na Said.

Magoli mawili ya kukamilisha ‘kiganja’ kwa Yanga yaliwekwa kambani na Amissi Tambwe dakika ya 65, na Kamusoko dakika ya 73.

Timu hizi mbili sasa zitarejeana wiki zijazo katika la Taifa jijini Dar es Salaam. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here