Home Kitaifa Manji ametajwa kwenye sakata la madawa ya kulevya

Manji ametajwa kwenye sakata la madawa ya kulevya

14506
0
SHARE

Jina la Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ni miongoni mwa majina 67 yaliyotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda yakiwa ni majina ya wanaoshukiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.

Makonda amesema wote waliotajwa kwenye orodha hiyo ya watu 67 wanatakiwa kuripo kwenye kituo cha kati (Central Police Station) siku ya Ijumaa kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Hii ni awamu ya pili Makonda anataja majina ya watu wanaoshukiwa kujihusisha au kutumia madawa ya kulevya baada ya awali watu 112 kukamatwa wengi wao wakiwa ni wasanii wa Bongofleva na Bongo Movies ambapo tayari baadhi yao wameachiwa kwa dhamana na kupewa masharti ya kuripoti polisi kila baada ya muda.

Watu wengine maarufu waliotajwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe, Askofu Josephat Gwajima sambamba na Mbunge wa zamani wa Kinondoni Idd Azzan.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here