Home Kitaifa Mambo 8 usiyoyajua kuhusu Himid Mao ‘Ninja’ wa Azam FC

Mambo 8 usiyoyajua kuhusu Himid Mao ‘Ninja’ wa Azam FC

12466
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

MAISHA ya mpira huenda kasi sana, dakika 90 pekee huweza kumfanya mchezaji awe mfalme au mtumwa katika timu. Shangwe na nderemo zinazozizima uwanjani kutokana na mapigo ya mpira kuwafurahisha wapenzi wa timu fulani, huenda sambamba na kipaji alichonacho mchezaji. Unapozungumzia mafanikio ya Azam FC, wapo wengi ambao huweza kutajwa.

Shuti  la mita 35 lilitosha kuhitimisha ndoto za wanasimba juu ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi wiki chache zilizopita visiwani Zanzibar. Aliyekatisha ndoto hizo ni kiungo Himid Mao ‘Ninja’ ambaye ndiye aliyekuwa shujaa kwa timu yake na kuipa ushindi timu ya Azam, mtandao wa shaffihdauda.co.tz   umemtafuta kiungo huyo na kuzungumza nae ambapo hapa antiririka kama ifuatavyo.

Historia yake.

Himid ni wa kwanza kuzaliwa katika familia yenye watoto watano. Ndugu zake wengine ni Femina, Rozmana, Faisal na Rahim.

Elimu yake ya msingi aliipata katika Shule ya Msingi Kiwandani, Turiani, Morogoro darasa la kwanza na la pili na kuhamia Karume ya Dar es Salaam na alisoma hadi darasa la sita. Alihama tena na kumalizia elimu ya msingi Shule ya Msingi ya Dk. Omary Ali Juma iliyopo Magomeni, Dar es Salaam kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Tabata ambako alimaliza kidato cha nne mwaka 2011.

Himid Mao ni mtoto wa nyota wa soka wa zamani, Mao Mkami ‘Ball Dancer’ aliyewahi kuwa mchezaji wa Pamba ya Mwanza, Mtibwa Sugar ya Turiani Morogoro na Moro United ya Morogoro.

Wadau wa soka wanakumbuka ‘Ball Dancer’, ambaye alipewa jina hilo na mtangazaji maarufu wa zamani wa Redio Tanzania, Charles Hillary.

Himid anafuata nyayo za baba yake kutokana na umahiri wake katika sehemu ya kiungo lakini kikubwa zaidi ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja.

Jina lake lilikuwa ni miongoni mwa wanasoka waliofanya  vizuri kwenye ulimwengu wa soka kwani alikuwa tegemeo kwenye timu za taifa za vijana wa chini ya miaka 17, 20 na 23.

Mtazamo wa Himid kuhusu chipukizi kwenye soka la kisasa

“Chipukizi wazuri na wana msaada kwetu, ukimuangalia Masoud Abdallah amekuwa anafanya vizuri kuliko wachezaji wote wa timu B amekuwa na msimu  mzuri,”

Vipi kuhusu kocha wake Iddi Cheche?

“Ni mtu mzuri ambae tumemzoea kama baba yetu ambae anatushauri mambo mengi sana kuhusu maisha pamoja na mpira unavyoendele katika karne hii”.

Bao lake bora kuwahi kufunga

“Bao bora nililowahi kufunga hadi sasa lilikuwa dhidi ya  Ruvu Shooting lilioisaidia timu yangu kuchukua ubingwa wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara”.

Nje ya soka Himid anapenda nini?

“Napendelea kulala na kucheza game (play station)”.

Kuhusu misosi je?

“Mimi sichagui wala sijivungi chakula, chochote  kinachokuja mbele yangu nakula”.

Umeoa?

“Nimeoa mke wangu anaitwa Hannan Abdulhafidh na tumebahatika kupata mtoto moja wa kike jina lake Balqis”

Rangi anazopenda Himid

“Nyeusi, Nyekundu, Nyeupe”

Unamiliki simu ya aina gani?

“iphone 6S”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here