Home Kimataifa Goli la Antoine Griezmann limeibeba Barcelona kucheza fainali Copa del Rey

Goli la Antoine Griezmann limeibeba Barcelona kucheza fainali Copa del Rey

18082
0
SHARE

Mara nyingi Atletico Madrid ilikuwa kwenye mlima mkali ilipocheza kwenye uwanja wa Camp Nou usiku wa Jumanne February 7, 2017 mchezo wao wa marudiano wa nusu fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona.

Magoli ya kuvutia kutoka kwa Luis Suarez na Leo Messi kwenye mchezo wa awali wiki iliyopita yaliiweka Barcelona kwenye nafasi nzuri licha ya Antoine Griezmann kutishia kuharibu ushindi wao.

Diego Simeone aliwekeza mbinu zake kwa washambuliaji kwenye mchezo wa marudiano pale Camp Nou lakini hata hivyo watoto hao wa mji mkuu wa Hispania bado hawakupata bao katika kipindi cha kwanza.

Licha ya kutawala mchezo, Leo Messi alitengeneza bao ambalo lilifungwa na Luis Suarez dakika tatu kabla ya kwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kilikuwa ni kama vita kutokana na matukio ya kibabe kutawala mchezo na kuharibu ladha ya game hiyo.

Dakika ya 57 Atletico ilipata ahueni huenda wangekuja juu baada ya mchezaji wa Barcelona birthday boy Sergi Roberto kulimwa kadi nyekundu kufatia kuoneshwa kadi ya pili ya njano.

Dakika mbili baadae kukatokea tukio lililozua utata ni baada ya Antoine Griezmann kufunga goli ambalo halikuwa na ubishi wowote lakini lilikataliwa na mwamuzi kwa kigezo kwamba goli hilo lilikuwa la offside.

Baadae ikiwa zamu ya Atletico kucheza pungufu kufatia Yannick Carrasco kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kadi ya pili ya njano huku Kevin Gameiro akipoteza mkwaju wa penati ambao ungeisawazishia bao Atletico.

Dakika ya 90 Luis Suares akachezea kadi nyekundu nay eye ikiwa ni baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano.

Bado wadau wanasema kwamba, goli la Griezmann lililokataliwa ndio limeibeba Barcelona kufuzu kucheza fainali ya Copa del Rey

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here