Home Ligi EPL Serie A Inapoamua Kuvamia Ligi Kuu Ya Uingereza.

Serie A Inapoamua Kuvamia Ligi Kuu Ya Uingereza.

4129
0
SHARE

Na Susy Campanale, Football Italia.

Kama ulitizama michezo ya wikiendi hii ya ligi kuu Uingereza unaweza kusamehewa kama ulihisi ilikuwa ni upande wa pili wa ligi kuu ya Italia. Alikuwepo Antonio Conte aking’ang’ana na mpira katika chaki kama vile anafunga. Upande mwingine Walter Mazzarri anashinda michezo yake akiwa na M’Baye Niang, Mauro Zarate na Roberto Pereyra. Manolo Gabbiadini alikuwa anafunga bao kali kwa upande wa Southampton kabla ya West Ham hawajasawazisha kupitia kwa mchezaji wa zamani wa Sampdoria Pedro Obiang.

Kwa miaka mingi tumeshuhudia vilabu vya Italia vishindwa kushikilia vipaji vyao,  ambazo uwauza kwenda ligi nyingine kwa fedha nyingi na mishahara mikubwa ambayo vilabu vingine vya Serie A haviwezi kufikia. Lakini hali inabadilika, wachezaji wanaotua nchi kama Uingereza sio wale mastaa na nyota tena bali walioshindwa kung’ara na kuendana na falsafa za Italia. Lakini bado wanaonekana kama vito vya thamani kwa mashabiki wa EPL.

Andrea Ranocchia alitangazwa kama mchezaji bora wa mechi katika mchezo ambao Hull City waliifunga Liverpool 2-0. Ranocchia hajawahi kuwa mchezaji bora katika mchezo wowote Italia. Ni maarufu kwa makosa mengi ya kijinga walau moja kila mchezo. Anacheza taratibu na muda mwingi alikutwa nje ya nafasi, huyu ndiye beki ambaye mashabiki wa Inter hawakuwahi kumkubali.

Niang alikuwa nyota wa mchezo wakati Watford inaichapa Burnley 2-1, akipiga krosi maridadi kwa Troy Deeney kabla ya baadae kufunga mwenyewe. Niang alifunga na kutoa pasi ya bao, haimaanishi kuwa hana kipaji, lakini Italia alitembulika kama mchezaji mwenye maamuzi mabovu ndani na nje ya uwanja. Iwe aliendesha bila leseni au kujifanya kuwa rafiki mzuri uwanjani lakini hatokupa pasi ilimradi abutue, huyu kwa Italia alikuwa mtu ambaye siku zote ungemtegemea kufanya makosa.

Inawezekana Premier League inamfaa Niang, kwa sababu hatowaza juu ya malalamiko ya makocha na mashabiki, kuhusiana na kurudi nyuma, kusaidia ulinzi, kufuata mbinu zilizowekwa na kujituma hata akiwa hana mpira. Kuna sababu nyingi kwanini mastriker hawafungi sana kwenye Serie A, sio kwa sababu ligi ya Italia ina ulinzi mkali au ni korofi. Kuweza kulinda sio kosa lakini inafanya kupatikana kwa magoli kuwe na maana zaidi.

Ni ngumu kusema kuwa Napoli wana ulinzi mkali au wanacheza kibabe. Ushindi wao wa 7-1 dhidi ya Bologna haikuwa kawaida, lakini mchezo wa pasi moja moja na wanavyoondoka ni vitu unavyoweza kuvifurahia kila wiki. Maurizio Sarri ni maarufu kwa kutokumchezesha mchezaji mpaka pale mbinu zake zinapowaingia akilini. Wachezaji wa Napoli hawapeani pasi, wanaupiga katika njia ambayo wanajua mchezaji mwingine atapitia.

Claudio Ranieri alisema akiwa na Leicester City alihitaji kuwapa mbinu, kama chakula tu kwenye sahani ya mtoto, kwa sababu vinginevyo wachezaji wangeshindwa kufuatana na muundo ambao angeuhitaji. Conte ana wachezaji wengi zaidi wa kimataifa kwenye kikosi cha Chelsea na siku zote mtizamo wake umekuwa katika miendendo kuliko mfumo. Kwenda kwenye umati na kukumbatia mashabiki ndicho alichoumbiwa Conte.

Sarri ni kama profesa wa mpira, anafanya kazi kwa nadharia zaidi na mabadiliko yanayotokea ndani yake. Inaweza ikaonekana ni ajabu lakini tizama Dries Mertens na Marek Hamsik wanavyopata kwa muda mmoja.  Juventus na Inter pia wanatumia mifumo ya kushambulia na kuburudisha. Ni ngumu kushutumu kikosi chenye Miralem Pjanic, Mario Mandzukic, Gonzalo Higuain, Paulo Dybala na Juan Cuadrado kwakuwa na mbinu za ulinzi.

Inawezekana baadhi ya wachezaji watafanya vyema kwenye Premier League na kufurahia kukosa sheria kila wakati, lakini ninapenda mbinu za Kiitalia. Kwa namna inavyokuwa ngumu kupata unachokitaka ndipo tunaporidhika.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here