Home Dauda TV VIDEO: Cameroon bingwa AFCON 2017

VIDEO: Cameroon bingwa AFCON 2017

6567
0
SHARE

February 5 ndio siku ambayo mchezo wa fainali ya kombe la mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2017 ulichezwa,  mchezo ambao ulikuwa ni maudio ya fainali ya mwaka 2008 kwa kuzikutanisha timu za Misri dhidi ya Cameroon, lakini Cameroon wamefanikiwa kufuta uteja kwa kufungwa fainali mbili na Misri.

Cameroon wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, magoli yakifungwa na Nicolas N’koulou aliyefunga goli la kusawazisha kwa Cameroon dakika ya 58 baada ya Mohamed Elneny kuifungia Misri bao la uongozi dakika ya 22 kipindi cha kwanza, Vincent Aboubakar akafuta ndoto za Misri kwa kupachika bao la pili na la ushindi kwa Cameroon zikiwa zimesalia dakika mbili pambano kumalizika.

Ushindi huo unakuja baada ya Cameroon kufumgwa fainali mbili za AFCON na Misri, walifungwa fainali ya AFCON 2008 kwa kipigo cha goli 1-0 la Mohamed Aboutrika, lakini mwaka 1986 walipoteza tena mchezo wa fainali.

Sasa Cameroon wanakuwa wamechukua taji lao la tano la AFCON huku Misri bado wakiendelea kuwa wababe wa taji hili wakiwa na rekodi ya kulichukua mara saba.

Cameroon imekuwa timu ya kwanza kutikisa nyavu za Misri  katika mchezo wa fainali za AFCON baada ya Ethiopia, huku kocha wa Misri Hector Raul  Cuper akiendeleza rekodi yake mbovu kwa kupoteza fainali yake ya sita katika soka akiwa kocha wa timu tofauti.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here