Home Kimataifa Watatu kumpisha Griezman Manchester United.

Watatu kumpisha Griezman Manchester United.

16248
0
SHARE

Baada ya usajili mkubwa msimu huu wa Paul Pogba Man United wanaonekana wanataka kufanya usajili mkubwa mwingine katika dirisha kubwa lijalo la usajili.Na sasa baada ya Paul Pogna timu ya United inahusishwa na kutaka kumchukua Mfaransa mwingine Antoine Griezman toka Athletico Madrid.

Lakini safari hii United wanataka kuuza baadhi ya majina makubwa ili kuweza kumnunua Griezman.Taarifa zinasema Manchester United watauza wachezaji wakubwa watatu ili kupata pesa za kuweza kumleta Griezman ambae thamani yake ni kubwa.
Tetesi zinasema Griezman ameshakubaliana na Man United kuhamia klabuni hapo kwa dau la £ 100m,huku akiingiza £15m kila mwaka katika mkataba huo.Pesa hizo zinaonekana nyingi sana na ili kujaribu kuweka sawa masuala ya malipo ni lazima baadhi ya wachezaji wakubwa wa United wapunguzwe ili kumpisha Griezman.
Inafahamika kwa sasa Athony Martial hayupo katika uhusiano mzuri na kocha Mourinho.Wakala wa Martial alishajaribu kumuuza mteja wake katika ligi ya Hispania japo jambo hilo halijawezekana lakini inaonekana wazi kwamba Martial anaweza kuwa mmoja ya wanaoondoka.Lakini pia Marouane Fellaini pamoja na kupewa nafasi na Mourinho bado hayupo katika kiwango kizuri na yeye anaweza kumfuata Martial.
United tangu kuondoka kwa kocha Alex Ferguson wamekuwa wakitumia kiasi kikubwa katika usajili.Tangu Ferguson aondoke Man United wametumia £ 513 katila usajili kiasi ambacho ni kikubwa kuliko kiasi walichotumia Real Madrid na Barcelona katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Mchezaji wa tatu ambae inasemekana anaweza kumpisha Griezman ni kapteni Wayne Rooney.Siku za karibuni Rooney amekuwa mchezaji wa akiba lakini pesa ndefu kutoka China zinaweza kuishawishi Manchester United kumuacha aende.Si hivyo tu lakini Rooney mshahara wake mrefu wa £ 300000 kila wiki inaweza kuwa sababu ya United kumpunguza Rooney ambae hata hivyo umri wake umeenda.
United wanapambana sana kurudisha ufalme wao uliopotea kwa muda sasa.Wanajaribu kusajili majina makubwa kwa pesa kubwa na katika kipindi hiki ambacho wachezaji wao muhimu wanaonekana umri kwenda,Griezman anaweza kuwa muarobaini wa tatizo la Manchester United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here