Home Dauda TV VIDEO: Burkina Faso imeitupa Ghana nafasi ya nne AFCON 2017

VIDEO: Burkina Faso imeitupa Ghana nafasi ya nne AFCON 2017

7184
0
SHARE

Free-kick ya dakika ya 89 iliyopigwa na Alain Traore ilimaliza ubishi wa Ghana na kuishuhudia Burkina Faso ikitangazwa kuwa mshindi wa tatu wa michuano ya AFCON 2017.

Kutoka upande wa kushoto wa box, Traore aliachia mkwaju kwa mguu wake wa kushoto ulio jaa moja kwa moja kwenye kona ya juu ya nyavu za Ghana.

Bao hilo likawaacha Ghana wakikamata nafasi ya nne kwa mara ya tatu katika michuano minne iliyopita ya Afrika.

Jordan Ayew, Edward Agyemang Badu na Bernard Tekpetey wote walipoza nafasi za kuifungia magoli The Black Stars.

Ni fursa ya Burkina Faso kujifariji kwa kushika nafasi ya tatu kufatia kushindwa kufuzu hatua ya fainali baada ya kuchapwa kwa matuta na Misri.

Usiku wa leo Misri inakutana na Cameroon kwenye mchezo wa fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here