Home Kimataifa Evra alikaribia kurudi united mwezi uliopita

Evra alikaribia kurudi united mwezi uliopita

3747
0
SHARE

Patrice Evra amerudi kwao Ufaransa katika klabu ya Marseille.Evra amerudi Ufaransa akitokea Juventus ya Italia,lakini hapo kabla kati ya mwaka 2006 na 2014 Patrice Evra aliichezea timu ya Manchester United na kushinda nayo makombe muhimu katika kipindi hicho.

Wakati wa usajiki wa dirisha dogo la mwezi uliopita ziliibuka tetes zilizozungumzwa sana kwamba Evra anarudi Manchester United.Uvumi huo ulienea haswa katika kipindi ambacho Man United wana tatizo la beki namba 3.Ilisemekana Jose Mourinho alikuwa katika hatua za mwisho kabisa kumrejesha Patrice Evra na kumfanya aungane na nyota wa zamani wa Juventus Paul Pogba.

Lakini dili hilo halikutokea na Pogba alienda Marseille.Sasa wakati juzi kati Evra aliporudi Italia kuwasalimia rafiki zake wa Juventus,alifanyiwa mahojiano na jarida maarufu la michezo nchini humo liitwalo Sky Italia na moja kati ya maswali aliyoulizwa ilikuwa kuhusiana na usajili wake kwenda United uliishia wapi.

Evra amekiri kwamba alikaribia kabisa kurudi Manchester United na alizungumza hadi na kocha wa timu hiyo Jose Mourinho kuhusu usajili huo.Lakini katika hali ambayo Evra hakuitarajia kuna mtu mmoja ndani ya Manchester United ambae hakumtaja jina aliamua kuzuia usajili huo kwa makusudi.

“Nilikaribia kabisa kujiunga na United,nilizungumza na kocha Mourinho lakini kuna mtu mmoja tu ambae siwezi kumtaja na huyu ndio alifanya usajili wangu kwenda United ushindikane” Evra aliiambia Sky Italia.Evra anaonekana bado anaipenda sana United na alitamani kurudi katika klabu hiyo ya zamani.

Evra aliongeza kuwa “mashabiki walifurahia sana tetesi za kurudi United na nilipoona hilo limeshindikana nilimuambia wakala wangu atafute timu nyingine”.Evra anasema baada ya hilo kushindikana ndipo walikuja Marseille na ilimchukua siku moja tu kukamilisha uhamisho huo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here