Home Kitaifa Timu yapigwa 8-0 ligi ya Zanzibar, Hilika kapiga hat-trick

Timu yapigwa 8-0 ligi ya Zanzibar, Hilika kapiga hat-trick

3198
0
SHARE

Na Abubakar Khatib ‘Kisandu’, Zanzibar

Baada ya mchezo uliopita kuvaa jezi sare na timu ya Mundu, na kuzikosa alama zote 3 pamoja na kupigwa faini ya shilingi 600,000 hatimae jana timu ya Kimbunga imejikuta inapata aibu nyingine baada ya kufungwa jumla ya mabao 8-0 kutoka kwa Zimamoto katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja uliopigwa saa 10 za jioni.

Katika mchezo huo nambari 170 ndio mchezo uliozaa magoli mengi kuliko yote ambapo Ibrahim Hamad Hilika akiondoka na mpira wake baada ya kupiga Hat-trick katika dakika ya 1, 27 na 64.

Mabao mengine ya Zimamoto yamefungwa na Hakim Khamis ‘Men’ dakika ya 40, 44, Khatib Said dakika ya 46, Idrissa Simai dakika ya 65 na Rashid Haji dakika ya 90.

Mechi nyingine zilizopigwa hapo jana mapema saa 8:00 za mchana Polisi na Chuoni walitoka sare ya 0-0, na mchezo wa usiku kati ya Jang’ombe Boys na Chwaka Stars wakamaliza kwa sare ya 1-1.

Chwaka ndio wa mwanzo kupata bao lililofungwa na Ali Hilali dakika ya 6 huku Hafidh Barik ‘Fii’ alisawazisha dakika ya 17 kwa upande wa Boys.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumamosi kati ya Kilimani City kukipiga na KMKM Saa 10:00 za jioni na mchezo mwingine Polisi dhidi ya Malindi saa 1:00 usiku.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here