Home Kitaifa Hat-trick yampaisha Hilika Zanzabar

Hat-trick yampaisha Hilika Zanzabar

4991
0
SHARE

Na Abubakar Khatib ‘Kisandu’,  Zanzibar

Mshambuliaji wa Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika jana amekuwa kinara kwa kucheka na nyavu baada ya kupiga Hat-trick timu yake iliposhinda 8-0 dhidi ya Kimbunga katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja uliopigwa katika dimba la Amaan.

Hat-trick hiyo imemfanya aongoze kwa kufunga mabao baada ya kufikisha mabao 11 akifuatiwa na mwenzake wa Zimamoto Hakim Khamis ‘Men’ mwenye mabao 10 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mudrik Muhib wa KMKM pamoja na Rashid Abdallah ‘Gaska’ wa Mafunzo ambao wote wana mabao 8 kila mmoja.

Msimu ulopita Hilika pia alipiga Hat trick katika hatua ya 8 bora ya ligi kuu soka ya Zanzibar ambapo Zimamoto iliposhinda 6-0 dhidi ya Afrika Kivumbi mchezo uliopigwa katika dimba la FFU Finya huko Kisiwani Pemba.

Jumla ya Hat trick 4 mpaka sasa zimeshafungwa katika ligi hiyo ambapo alianza mshambuliaji wa zamani wa Jang’ombe Boys Abrahman Othman ‘Chinga’ ambaye kwasasa anacheza Singida United ligi daraja la kwanza Tanzania bara, na Hat trick ya pili ikafungwa na Khamis Maulid wa Polisi, ya tatu ikapigwa na Mshambuliaji wa timu ya Kipanga David Julius Nyerere ‘Chope’ na ya nne ndio hiyo ilopigwa na Hilika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here