Home Kitaifa Mchezaji wa zamani wa Yanga na Stars yupo hoi kitandani…

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Stars yupo hoi kitandani…

6814
0
SHARE

Tangu jana jioni kumekuwa na taarifa sambamba na picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kueleza hali ya kiafya ya Godfrey Bonny mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars.’

Godfrey Bonny amelazwa hospitali huko Rungwe-Tukuyu Mbeya ambako anapatiwa matibabu, jana Sports Extra ya Clouds FM ilizungumza na mdau wa soka ambaye aliwasiliana na dada yake Boni ambaye ndio anamuuguza kwenye hospitali ya Rungwe.

“Nimezungumza na dadayake Gedfrey Bonny anaitwa Neema Boniface amenifahamisha kwamba hali ya kaka yake (Godfrey) Bon si nzuri kabisa na kwa sasa hawezi hata kuzungumza. Nimemuuliza kuhusu taarifa za daktari amesema kwamba atapewa majibu ya X-ray siku ya kesho (leo) lakini hali yake si nzuri kwa sababu hawezi kuzungumza,” mdau aliyezungumza na dada yake Bon aliiambia Sports Extra.

“Kiujumla ni kwamba hali ya Godfrey Bonny sio nzuri kwa sababu nimezungumza na dada yake anaishia kulia na kunifanya nishindwe kupata majibu ya moja kwa moja.”

Kama una kiasi chochote au mchango wowote, unaweza kuwasiliana na dada yake Bonny au kutuma kwenye namba 0765 329 290 ya Neema Bonidace ambae ni dada yake Godfrey Bonny.

Mtandao huu umeona si busara kutumia picha za mgonjwa ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimwonesha akiwa amelazwa hospitali.

Bonny aliwahi kuvitumikia vilabu vya Tanzania Prisons na Yanga kwa vipindi tofauti pamoja na timu ya taifa ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

shaffihdauda.co.tz inaungana na wadau wengine wa soka na michezo kwa ujumla kumtakia kila la heri Godfrey Bonny katika matibabu yake ili apone na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here