Home Kimataifa UEFA Wanataka Nafasi Zisizopungua 16, Kombe la Dunia 2026.

UEFA Wanataka Nafasi Zisizopungua 16, Kombe la Dunia 2026.

621
0
SHARE

Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA), Aleksander Ceferin ameweka wazi kuwa watahitaji kuwa na wawakilishi walau 16 kati ya nafasi  48 zitakazokuwepo kwenye mashindano ya kombe la dunia mwaka 2026. Akizungumza na Die Welt alisema: “sisi sio chama cha soka cha bara jingine.”

Halmashauri ya FIFA iliweka bayana mipango ya kuongeza timu kutoka 32 mpaka 48 kufikia mwaka  2026, ikiwa ni ongezeko la mataifa 16, na FIFA wanatarajiwa mpaka kufikia mwezi May kuweka bayana idadi ya nafasi za ziada ambazo kila bara litapata, na mabara kama ya Asia na Africa yakitegemewa kuongeza nafasi zaidi.

Ulaya kwa sasa wana nafasi 13 kwenye kombe la dunia na Ceferin alisema: “UEFA ilikuwa ni shirikisho pekee ambalo halikuhitaji mabadiliko haya, lakini hatukuwa na namna.

“Na ndio maana tumeamua kupigana kupata nafasi nyingi kadiri itakavyowezekana.”

Italia, Hispania na Ujerumani wameshinda mataji matatu yaliyopita ya kombe la dunia na kila kombe limechukuliwa na Taifa la kutoka Ulaya ama Amerika ya Kusini.

“Ubora upo Ulaya na Amerika ya Kusini, ,” alisema Rais huyo wa UEFA. “Hivyo ndivyo ilivyo. Tunahitaji walau nafasi 16, na hiyo itakuwa hali ambayo bado ni mbaya.”

UEFA pia ambayo ndicho chama cha vilabu chenye nguvu zaidi pia kimekuwa mstari wa mbele kupinga utaratibu huu mpya wa FIFA na kombe la dunia huku mwenyekiti wake ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge akiwataadharisha FIFA kuwa mapinduzi yanaweza yasiepukike.

Rummenigge alisema vilabu vinaweza kuwakatalia wachezaji kutokuondoka vilabuni kwa ajili ya kombe la dunia mwaka 2026 kwa kuhofia kuumia kwao ama kutumika kupita kiasi.

Ceferin alisema: “Tulikutana na [Rummenigge] mara kadhaa, na ninaoona vitu anavyoviona yeye.”

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here