Home Dauda TV VIDEO: Goli la Morocco lililoivua ubingwa Ivory Coast

VIDEO: Goli la Morocco lililoivua ubingwa Ivory Coast

878
0
SHARE

Morocco

Morocco imewavua ubingwa Ivory Coast baada ya kuwafunga goli 1-0 na kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi C kisha Morocco kufuzu kucheza robo fainali ya michuano hiyo mikubwa ya soka la Afrika kwa timu za taifa.

Shuti la Rachid Alioui akiwa umbali wa mita 25 liliipa Morocco ushindi pamoja na kocha wao Herve Renard, ambaye aliiongoza Ivory Coast kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka 2015.

Ivory Coast ilihitaji ushindi ili kufuzu hatua ya robo fainali lakini kiwango chao cha chini kwenye mchezo dhidi ya Morocco kiliwafanya watengeneze nafasi zisizozidi mbili ambazo pia walishindwa kuzitumia kupata magoli.

Morocco waliingia kwenye mechi hiyo wakijua, matokeo ya sare yalikuwa na maana kubwa kwao kufuzu kutoka Kundi C lakini walifanikiwa kupata ushindi kutokana na mchezo wao wa kujilinda na kutengeneza mashambulizi ya kushtukiza.

Morocco watacheza na kinara wa Kundi D kwenye mechi ya robo fainali inayotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili.

DR Congo pia wamefuzi kutoka Kundi C wakiwa vinara wa kundi baada ya kuichakaza Togo ya Vicent Bossou kwa bao 3-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here