Home Ligi EPL GUARDIOLA: Niongezeni Miaka 5.

GUARDIOLA: Niongezeni Miaka 5.

997
0
SHARE

Guardiola-Man City

Hatimaye kocha wa klabu ya Manchester City ni kama amegundua kuwa kazi ya kuijenga klabu ya Manchester City haiwezi kuwa rahisi. Guardiola kaamini kuwa kuiweka Man City katika kiwango anachohitaji ni kazi kubwa kuliko ilivyokuwa inadhaniwa awali.

Na hii inamaanisha kuwa Guardiola anasemekana kuhitaji muda zaidi wa kufanya yale ambayo alitaka kuyafanya katika klabu hiyo ya Manchester City.

Guardiola, 46,  yupo katika wakati mgumu kwa sasa kutokana na timu anaoifundisha kuwa katika nafasi ya 5 huku wakiwa na pointi 12 nyuma ya viongozi wa ligi Chelsea.

Ingawa pia kumekuwa na taarifa kuwa kocha huyu anaweza kuwa moja kati ya makocha wachache wanaoweza kushuhudia wakiondoka mapema zaidi kwenye vilabu vyao zaidi ya ilivyokadiriwa.

Hata hivyo vyanzo vya karibu vya klabu ya Manchester City pamoja na familia yake wamedai kuwa wameanza kuzoea maisha yao mapya huku kocha mwenyewe akisemekana kufurahia kazi yake.

Na taarifa zaidi zinadai kuwa kocha huyo anapata sapoti kubwa kutoka kwa tajiri na mmiliki wa klabu hiyo Sheikh Mansour pamoja na mikasa inayoendelea.

Haya yote inasemekana aliambiwa siku aliyokuwa na mkutano ambao haukuwekwa wazi na mwenyekiti Khaldoon Al Mubarak na viongozi wengine wa juu baada ya kutoka sare siku ya Jumamosi ya mabao 2-2 dhidi ya Tottenham.

Guardiola ameanza kujipanga kuwaacha baadhi ya wachezaji ikiwemo Joe Hart, Samir Nasri, Wilfried Bony and Eliaquim Mangala wote wakionyeshwa njia ya kutokea.

Hii itamaanisha kuwa zaidi ya kiasi cha paundi Milioni moja (£1million) kitaondolewa kwenye vitabu vya hesabu za mishahara za kila wiki.

Lakini pia kuna idadi ya wachezaji wengine saba wanaofikia ukomo wa mikataba yao ikiwemo Yaya Toure, Pablo Zabaleta and Bacary Sagna na wengine wanaoondoka kikosini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here