Home Dauda TV VIDEO: Tunisia ilivyooinyoosha Zimbabwe na kufuzu robo fainali AFCON 2017

VIDEO: Tunisia ilivyooinyoosha Zimbabwe na kufuzu robo fainali AFCON 2017

742
0
SHARE

Tunisia vs Zimbabwe

Tunisia imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika baada ya ushindi wao wa magoli 4-2 dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi B.

Shuti la Naim Sliti ambalo liliwababatiza mabeki wa Zimbabwe liliiandikia Tunisa bao la kuongoza kabla ya Youssef Msakni na Taha Khenissi kuongeza magoli mengine mawili ya kuongoza.

Knowledge Musona akaipatia Zimbabwe bao la kwanza lakini mkwaju wa penati wa Wahbi Khazri ukaongeza mlima kwa Zimbabwe.

Tendai Ndoro akapambana kuifungia Zimbabwe bao la pili kwa shambulizi la kushtukiza kabla ya shuti la Khenissi kugonga post wakati wa kipindi cha pili cha mapambano.

Mabingwa hao wa mwaka 2004 watakutana na Burkina Faso siku ya Jumamosi kwenye mji mkuu wa Gabon, Libreville.

Tunisia walihitaji sare tu ili kufuzu kucheza hatua ya robo fainali baada ya ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Waarabu wenzao Algeria siku ya Alhamisi iliyopita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here