Home Kimataifa Hii ni barua ya Ronaldinho kwa Gaucho.

Hii ni barua ya Ronaldinho kwa Gaucho.

1507
0
SHARE

dinho

Ronaldinho Gaucho moja kati ya vipaji vya soka bora kabisa kuwahi kutokea duniani mzaliwa wa Porta Alegre nchini Brazil mwaka 1980.Kipaji chake cha soka ameshakua kombe la dunia na timu ya taifa ya Brazil mwaka 2002 akichukia La Liga mara mbili na Barcelona na pia kombe la UEFA na pia akiwa amewahi kuchukua tuzo binafsi kama Ballon D’Or mwaka 2005 na ile ya UEFA mwaka 2005.

Gaucho amejiandikia barua,barua ambayo inaelezea mambo mengi aliyopitia katika soka lake na mambo ya kifamilia,katika barua hiyo Ronaldinho amejivika uhusika wa kaka yake Roberto kama anamuandikia Barua Ronaldinho mwenye miaka 8,ameelezea mengi kuhusu soka tangu amaamza soka katika klabu ya Gremio hadi anaenda Ulaya pia jina la Lioneil Messi limetokea kwenye barua hii,shaffih dauda inakuletea barua nzima ya Dinho.

Kwako Ronaldinho,kesho ukirudi nyumbani kutoka kucheza mpira utakuta watu wengi nyumbani marafiki wa familia,ndugu zako na watu wengine usiowajua watakuwa jikoni,unaweza kufikiri kuna sherehe ya kuzaliwa kwa kaka yako Roberto,kila ukitoka mpirani huwa unamkuta mama anacheka na kuwa na utani mwingi ila leo analia.

Utamuona kaka yako akikukumbatia na kukupeleka bafuni halafu atakuambia kitu usichotarajia,kumetokea ajali na baba amekufa,hutaelewa anamanisha nini?na hutajua baba anarudi lini?baba amekufaje?hutaelewa kwa sasa kwa kuwa umdogo lakininutakuja kuelewa.

Baba ndiye aliyekuambiwa ucheze kibunifu uwanjani na kuuchezea mpira,alikuamini kuliko mtu yeyote yule.Pale Roberto alipoanza kucheza mpira wa kulipwa pale Gremio mwaka jana baba aliwaambia watu Roberto ni mchezaji mzuri ila mutamuona mdogo wake(Ronaldinho)baba alikuwa shujaa.

Alipenda mpira hadi akimaliza kazi zake kwenye yadi ya meli alikwenda kufanya kazi za ulinzi kwenye timu ya Gremio,itakuwaje hutamuona tena?huwezi kuelewa Roberto asemacho,miaka michache ijayo utaelewa baba hatarudi tena duniani ila kila muda mpira ukiwa mguuni mwako jua baba yuko na wewe,mpira ukiwa mguuni mwako unakuwa huru na mwenye furaha kama vile unasikiliza muziki na hisia hizo zitakufanya utamani kusambaza furaha hiyo kwa watu wengine

Una bahati kwa kuwa Roberto yupo japo kakuzidi miaka 10 na tayari anacheza soka Gremio ila atakuwa msaada kwako,atakuwa wa thamani sana kwako na shujaa wako,ukichezea timu ya vijana ya Gremio yeye tayari atakuwa timu ya wakubwa na ukienda kitandani utawaza unaenda kukaa chumba kimoja na mtu muhimu kwako.

Hakuna mabango kwenye ukuta ila kuna kajivideo ila haijalishi kwa kuwa hamtakuwa na muda kuangalia mechi yoyote pamoja kwani asiposafiri Roberto atakupeleka nje kucheza mpira,unapoishi Porto Alegre kuna biashara za madawa ya kulevya na makundi ya kihuni ni mazingira magumu kuishi ila kwa kuwa unacheza mpira mtaani na mbwa wako utajihisi huru na salama,nasema mbwa kwa sababu ni mlinzi asiyechoka.

Utacheza na Roberto na vijana wengine kila mtu atachoka ila utaendelea kucheza kwahiyo hakikiaha unakuwa na mbwa wako Bombom kila muda,Bombom ni mbwa wa Kibrazil asiyechoka na mbwa wa Brazil pia wanapenda soka atakusaidia kufanya mazoezi kuuchezea mpira,miaka michache ijayo ukiwa Ulaya baadhi ya mabeki watakufanya umkumbuke Bombom.

Utoto wako utakuwa tofauti sana ukiwa na miaka13 watu wataanza kukuzungumzia wakizungumzia ufundi wako katika soka kwa sasa soka ni mchezo tu kwako ila ukiwa na miaka14 kombe la dunia litakuonesha kwamba soka ni zaidi ya mchezo,17 July 1994 ni siku kila Mbrazil anaikumbuka,siku hiyo utasafiri na Gremio kwa ajili ya mechi dhidi ya Belo Herizonte,kombe la dunia litakuwa kwenye video na ni Brazil dhidi ya Italia kila sehemu ya Belo Herizonte kutakuwa na bendera ya taifa ni kijani na njano tu hakuna rangi nyingine.

Utaangalia na wachezaji wako na mechi itaisha kwa suluhu ya bila kufungana,Italia walikosa penati ya kwanza,Brazil wakakosa pia,Italia wakafunga,Romario akapiga mpira uliogonga mwamba na kwenda kimiani,Italia wanafunga tena kisha Branco alitupatia goli,Taffarel akaokoa penati ya Waitalia,Dunga akafunga,hiyo siku inaishi kwenye mioyo yetu Wabrazil Roberto Bagio aligonga mwamba akakosa penati tukashinda kombe la dunia.

Katika kushangilia itakuonesha ni jinsi gani Wabrazil tunapenda soka utaona nguvu ya michezo,utaona furaha inavyoletwa na soka,utasema utatamani kuichezea Brazil,kuna makocha wataamini unachofanya wengine watakuambia uongeze juhudi na kukukatisha tamaa,tumia maneno hayo kukuhamasisha na waza kuhusu wachezaji wakubwa waliovutia kwenye soka kama Ronaldo,Deener na Maradona,waza kuhusu maneno ya baba ucheze mpira huru na kwa furaha japo makocha wengi hawatakuelewa kila kitu kotakuwa sawa,ubunifu utakufanya uwe bora.

Siku moja kocha wa Gremio atakuita ofisini na kukuambia umeitwa kwenye kikosi cha Brazil chini ya miaka 17,utaanza kula vyakula walivyokula wachezaji wakubwa na kula migahawa waliyowahi kula wakati wa mazoezi,ukilala usiku utawaza umelala mto ambao mchezaji gani mkubwa aliwahi kulalia,ukifikisha miaka 18 utapata kitu ambacho baba atajivunia sana kuhusu wewe utaanza kuchezea timu ya wakubwa ya Gremio ila Roberto hatakuwepo,siku za mechi utapitia sehemu ya kupaki magari ambapo baba yako aliwahi kufanya kazi za ulinzi.

Mwaka unaofuata utaanza kuichezea timu ya wakubwa ya Brazil,jambo la kuchekesha utachelewa mazoezini kwa kuwa utakuwa na Gremio kwenye fainali za Campeonato dhidi ya Internacional,watu waatanza kukuzungumzia muone yule dogo anayevaa jezi namba 10 anavyotembea na mpira,wataanza tarajia makubwa toka kwako ninakushauri endelea kufanya na kucheza unavyoamini kuchezea Brazil milango itafunguka.

Utaanza kuwaza Ulaya ukiambiwa kuhusu Ulaya na kuona tuzo ya Ronaldo ya dunia ya mwaka 2001 utaenda Ulaya kusaini PSG,ukiondoka PSG utaenda Barceloma halafu Milan mambo yatabadilika harakaharaka sana na baadhi ya vyombo vya habari Ulaya hawataelewa uchezaji wako wa mpira hawataelewa unavyotabasamu kila muda,unatabasamu kwa ajili ya soka kuwa huru ili ushinde kombe la dunia,kuwa huru tashinda La Liga na Uefa,kuwa huru utashinda Ballon d’or.

Ukiwa Barcelona utasikia kuhusu huyu kijana timu ya vijana anavaa jezi namba 10 kama wewe ni mdogo kama wewe ma anacheza kama wewe mutaanza kumuona kama mchezaji bora ajaye anaitwa Leo Messi utamuomba kocha amlete timu ya wakubwa,mshauri muambie acheze mpira kwa furaha,huru acheze mpira,mambo mengi mazuri na mabaya yatakutokea,hutamsikia tena baba ila ndio iwe kumbumumbu yako ya staili yako ya mpira

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here