Home Kitaifa Agyei ameyasema aliyoambiwa na Manyika Jr kabla ya ‘matuta’ vs Yanga

Agyei ameyasema aliyoambiwa na Manyika Jr kabla ya ‘matuta’ vs Yanga

1025
0
SHARE

dsc_0242

Camera ya shaffihdauda.co.tz ilinasa picha ya golikipa namba mbili wa Simba Manyika Jr akimnong’oneza jambo golikipa mwenzake Mghana Daniel Agyei wakati timu yao ikielekea kwenye changamoto ya penati dhidi ya Yanga.

Agyei alifanikiwa kuokoa michomo miwili ya penati zilizopigwa na Deogratius Munishi ‘Dida’ na Haji Mwinyi na kuisaidia timu yake ya Simba kufuzu hatua ya fainali ya Mapinduzi Cup 2017.

Baada ya mchezo nikaona isiwe tabu, nikamtamfuta Agyei kutaka kujua aliambiwa kitu gani na Manyika Jr.

“Manyika alikuwa ananiambia kuhusu upigaji wa penati wa baadhi ya wachezaji wa Yanga kwa sababu yeye anawafahamu vizuri kuliko mimi,” anasema Agyei ambaye alisajiwa wakati wa dirisha dogo la usajili na baadae kuchukua nafasi ya Vicent Angban baada ya kutoswa na Simba.

“Aliniambia kuhusu upigaji wa mchezaji anayevaa jezi namba 27 (Msuva) kwamba hupendelea kupiga upande wa kulia lakini ilipofika zamu yake alipiga katikati akanifunga.”

“Lakini akaniambia pia kuhusu mchezaji anaevaa jezi namba 20 (Haji Mwinyi) kuwa anatumia mguu wa kushoto kwahiyo kama atapiga basi niwe makini na uapande wangu wa kushoto na ndivyo ilivyotokea nikacheza penati yake.”

“Namshukuru sana Manyika naamini tutaendelea kushirikiana kuhakikisha tunafanikisha malengo ya klabu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here