Home Kitaifa Vitu 5 vya kujua kuelekea Simba vs Yanga Mapinduzi Cup2017

Vitu 5 vya kujua kuelekea Simba vs Yanga Mapinduzi Cup2017

1566
0
SHARE

simba-vs-yanga-2

January 10, 2017 Simba na Yanga zinakutana kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar. Mechi inatarajiwa kuanza saa 2:15 usiku ikiwa ni nusu fainali ya pili baada ya mechi ya kwanza kati ya Azam vs Taifa Jang’ombe ambayo itachezwa kuanzia saa 10:15 jioni.

Kuelekea mchezo wa nusu fainali kati ya Simba vs Yanga, nimekuandalia mechi saba zilizopita zilizozikutanisha timu hizi kwenye ligi kuu Tanzania bara.

Katika mechi hizo, Yanga imeshinda mechi mbili, Simba imeshinda mara moja huku timu hizo zikitoka sarekwenye michezo minne.

Simba vs Yanga uso kwa uso

10/01/2017 Yanga ?? Simba

01/10/2016 Yanga 1-1 Simba

20/02/2016 Yanga 2-0 Simba

26/09/2015 Simba 0-2 Yanga

08/03/2015 Simba 1-0 Yanga

18/10/2014 Yanga 0-0 Simba

19/04/2014 Yanga 1-1 Simba

20/10/2013 Simba 3-3 Yanga

Kocha wa Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina atasimama kwenye benchi la ufundi kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya Simba na Yanga tangu alipoajiriwa kwenye timu hiyo kuchukua nafasi ya Hans van Pluijm.

Wageni Simba vs Yanga

Yanga

Emanuel Martin, Justine Zulu ‘Mkata umeme’ kama wakicheza mechi ya leo, watakuwa wanacheza kwa mara ya kwanza mchezo wa watani wa jadi tangu walipojiunga na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili wa msimu huu.

Simba

Pastory Athanas, Juma Liuzio, James Kotei, Daniel Agyei , endapo watacheza mechi ya leo dhidi ya Yanga itakuwa ni mechi yao ya kwanza ya mahasimu wa soka la Bongo.

Zilipotoka Mapinduzi Cup 2017

Simba ilipangwa Kundi A lililokuwa na timu tano (Simba, Taifa Jang’ombe, Jang’ombe Boys, URA, KVZ) Simba ikapita kwenda nusu fainali ikiwa na pointi 10 ikifuatiwa na Taif Jang’ombe Boys yenye pointi tisa.

Simba ilishinda mechi zake tatu na kutoka sare mechi moja kati ya mechi nne za Kundi A, ilifunga jumla ya magoli matno huku ikiwa imefungwa goli moja pekee.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC yenyewe ilikuwa Kundi B ambalo lilikuwa na jumla ya timu nne (Azam, Yanga, Zimamoto na Jamhuri) Azam ikamaliza kinara wa kundi hilo ikiwa na pointi 7 ikifatiwa na Yanga yenyepointi sita ambazo zilifuzu hatua ya nusu fainali.

Yanga imeshinda mechi mili kwenye hatua ya makundi na kupoteza mchezo mmoja. Imefunga magoli nane na kuruhusu magoli manne.

Ubingwa wa Mapinduzi Cup

Tangu mwaka 2007 Simba na Yanga zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi mara tatu.

Simba imetwaa mara mbili kati ya mara hizo tatu. Mwaka 2007 Yanga walichukua kombe hilo lakini mwaka 2008 kombe likaenda mitaa ya msimbazi. Simba ikalichukua tena mwaka 2015 kwa mara ya mwisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here