Home Kimataifa Uwanja wa Maracana wang’olewa viti zaidi ya 7,000.

Uwanja wa Maracana wang’olewa viti zaidi ya 7,000.

631
0
SHARE

screen-shot-2017-01-10-at-5-46-17-pm
Kwa wewe ambae ulifuatilia mechi za kombe la dunia basi uwanja wa Maracana lazima utakuwa kwenye kumbukumbu zako hasa mechi ya fainali kati ya Argentina Vs German. Mechi ile ilimalizika kwa kupigwa fataki ambazo zilipendezesha jiji la Rio.

Uwanja wa Maracana ulijengwa mwaka 1950 na kufanyiwa ukarabati kabla ya kufanyika kombe la dunia kwa gharama ya kiasi cha £500million. Lakini sasa hivi hali yake ni mbaya kiasi kwamba hauwezi kutumika kwa mechi za mashindano tena.

Ripoti zinasema kwamba  uwanja huo umeng’olewa viti zaidi ya 7,000 na kuacha sehemu nyingi zikiwa na mapengo tofauti na ulivyokua mwanzo. Uwanja huu pia ulitumika kipindi cha Olympics na kamati ya Maracana inasisitiza kwamba kamati ya Olympics ina majukumu ya kukarabati uwanja huo ndio wakabidhiwe wao.

Kutokana na utata huo ambapo hakuna pande yoyote kati yao wanaosimamia manitainance ya uwanja huo kwa sasa basi unazidi kuharibika. Hizi ni picha za uharibifu wa uwanja huo kwa jinsi ulivyo sasa hivi.

screen-shot-2017-01-10-at-5-46-10-pmMajani yameota nje ya uwanja

screen-shot-2017-01-10-at-5-45-59-pm

Ndani ya uwanja majani yameng’oka

 

screen-shot-2017-01-10-at-5-45-52-pm

Viti vimeng’olewa na vingine vimeng’oka kama unavyoona

screen-shot-2017-01-10-at-5-45-45-pm

Baadhi ya viti vilivyong’oka na kuweka store na vingine vimesha potea

screen-shot-2017-01-10-at-5-45-39-pmSehemu za paa za uwanja huo kuanzia ndani hadi sehemu nyingine zina hali mbaya

screen-shot-2017-01-10-at-5-45-18-pm screen-shot-2017-01-10-at-5-45-09-pm

Nyavu za magoli nazo zina hali mbaya kupita kiasi.

screen-shot-2017-01-10-at-5-45-31-pmMiezi michache iliyopita uwanja huu ulipendezeshwa na sherehe  za Olympics.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here