Home Kimataifa Sanamu Ya Messi Yavunjwa Argentina

Sanamu Ya Messi Yavunjwa Argentina

754
0
SHARE

messi

Sanamu ya nchezaji wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi imekutwa imevunjwa huko katika mji wa Buenos Aires siku ya Jumatatu/

Sanamu hiyo ilijengwa ili kumshawishi Messi ili aondoe uamuzi wake wa kustaafu kuchezea timu ya Taifa na kurejea kikosini. Sanamu hiyo ilikutwa haina nusu yake ya juu.

Hata hivyo watendaji na viongozi wa soka nchini humo wamesema tayari wameanza utaratibu wa kuirejesha kwenye hali yake ya kawaida.

messi-vs-celtic

“Sanamu hiyo ya Lionel Messi imekutwa imevunjwa na taarifa za awali zinasema ni uvunjaji wa makusudi ambao hauhusiki na vuguvugu zozote za kisoka au kisiasa,” mamlaka za serikali na jiji za Buenos Aires zilisema kwenye taarifa.

“urekebishaji wake kwa sasa upo kwenye mkakati na umeanza kufanyika.”

Sanamu hiyo ipo katika eneo maarufu la “Paseo de la Gloria” akiwa pamoja na wanamichezo wengine kama mcheza tenisi Gabriela Sabatini na mchezaji wa NBA na bingwa wa Dunia, Manu Ginobili akiwa miongoni mwao wenye sanamu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here