Home Kitaifa Potezea kuhusu Mkwasa na Ongala, Azam imeleta kocha kutoka Romania

Potezea kuhusu Mkwasa na Ongala, Azam imeleta kocha kutoka Romania

913
0
SHARE

20170110_151033

Baada ya kutimua makocha raia wa Hispania, klabu ya Azam FC imeshusha kocha mpya anaejulikana kwa jina la Aristica Cioaba kutoka Romania.

Kocha huyo amepewa mkataba wa miezi sita kwa ajili ya matazamio kama atafanya vizuri huenda akapewa mkataba wa muda mrefu lakini kinyume na hapo atafata nyayo za akina Zeben Hernandez.

Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd amesema Aristica Cioaba atasaidiwa na makocha wazalendo ambao wanaiongoza Azam kwa sasa wakiongozwa na Idd Cheche.

“Tumeshapata kocha mpya kutoka Romania ambaye tumempa mkataba wa miezi sita ili tuweze kuangalia uwezo wake. Kama atafanya vizuri basi tunaweza kumuongezea muda,” anasema Jafar Idd uku akiziua tetesi za makocha wazawa kujiunga na Azam.

“Kwa sasa atakuwa akisaidiwa na makocha wetu wazalendo ambao wapo na timu wakiongozwa na Idd Cheche.”

Baada ya Zeben na wasaidizi wake kutimuliwa, ziliibuka tetesi kuwa huenda Karl Ongala ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo akiwa mchezaji na kocha msaidizi akarejeshwa kwenye benchi la ufundi la Azam FC.

Mkwasa pia ni miongoni mwa makocha waliotajwa kupewa jukumu la kuinoa Azam baada ya kuachana na timu ya taifa ya Tanzania lakini ujio wa Aristica Cioaba unamaliza tetesi hizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here