Home Kitaifa Yanga imetupa morali – John Bocco

Yanga imetupa morali – John Bocco

953
0
SHARE

screen-shot-2017-01-09-at-9-26-41-pm

Nahodha wa kikosi cha Azam FC John Bocco amesema ushindi wa mabao 4-0 umewapa morali kuelekea mchezo wao wa nusu fainali ya mapinduzi Cup dhidi yaTaifa Jang’ombe.

Bocco amesema mechi dhidi ya Taifa Jang’ombe huenda ikawa ngumu kuliko hata mechi yao dhidi ya Yanga kwa sababu wanacheza na timu ambayo ipo nyumbani jambo ambalo linaweza kuwapa changamoto.

“Tumefanya vizuri mazoezi yetu ya yetu ya mwisho wachezaji wapo kiatika hali nzuri ya kiafya ukizingatia mchezo wetu uliopita tulipata ushindi kwa hiyo morali yetu iko juu sana kubwa tunaangalia mchezo huo ambao utakua mgumu pengine kuliko hata mchezo wetu uliopita Jang’ombe ni timu nzuri pia ni timu ya hapa Zanzibar wanamashabiki wengi inaweza kuwa challenge kwetu kujituma kupata ushindi.”

“Tunaheshimu wapinzani wetu tunaoenda kukutana nao na kikubwa tutajituma sisi kama wachezaji ili kupata ushindi,” anasema Bocco mfungaji wa bao la kwanza kwenye mechi dhidi ya Yanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here