Home Kimataifa Wakala wa Patrice Evra azungumzia kuhusu link ya Evra na United.

Wakala wa Patrice Evra azungumzia kuhusu link ya Evra na United.

453
0
SHARE

evra

Moja ya story ambazo hazikutegemewa sana ni story za kwamba Patrice Evra atajiunga na Manchester united club ambayo amecheza kwa muda mrefu na kupata mafanikio.

Ukweli ni kwamba Evra atasepa Juventus lakini sio kwa ajili ya kwenda kucheza Manchester United. Wakala wake Federico Pastorello amesema kwamba sio swala la kuficha kwamba Evra ataondoka Juventus, tutaona ndani ya siku chache zijazo.

Habari zinasema kwamba Manchester United inaweza kumpa Evra nafasi ya kuanza career ya kuwa kocha. Inategemewa kwamba mwishoni mwa msimu huu ndio itakua mwisho wake na ataacha kucheza soka la mashindano.

Uhusiano wake mzuri na Paul Pogba na Antoine Griezmann unampa sababu nyingi Evra kuwa kwenye timu ya Jose Mourihno. Griezmann bado ni chaguo la Jose Mourihno na pia kuna mchezaji gani ambaye hatapenda kuanza kuwa kocha akiwa chini ya Jose Mourihno kocha mwenye mafanikio.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here