Home Kitaifa Waambieni Simba Yanga Ndio Mabingwa

Waambieni Simba Yanga Ndio Mabingwa

1073
0
SHARE

hhhh
Kesho tukielekea kwenye mechi nzuri kati ya Simba Vs Yanga ni wakati mzuri kuweka mbele msatari wa msanii Young Killer kwenye ngoma yake mpya inaitwa Sinaga Swaga.
Young Killer ijulikane kwamba yeye ni mpenda soka na ndoto yake ya kwanza ilikua ni kucheza soka zaidi ya kuwa mwanamuziki.

Young Killer aliwahi kuwa kwenye academy ya soka akiwa kwenye harakati za kutaka kuwa mchezaji soka hapo mbeleni. Mara nyingi Young Killer ameonekana kwenye mechi za Yanga na kuonyesha mapenzi yake ya dhati kwamba yeye ni shabiki namba moja wa Yanga.killer

Kwenye ngoma hii ametumia sanaa yake kusema kwamba “Wambie Simba Yanga Ndio Mabingwa, Kauli ya kujipanga siku zote ni dalili ya kushindwa”. Oky sasa hiyo ni sanaa tu lakini pia Killer ni shabiki mwenzetu wa soka na upenzi wake wa Yanga usichanganywe na muziki wake. Tusubiri kesho kama atalia au atacheka baada ya club yake kucheza kwenye kombe la Mapinduzi. Hii hapa ni video mpya ya Young Killer ambayo kuna mstari huo ndani yake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here