Home Kimataifa Nyumba ya Roberto Firmino yavamiwa na kuibiwa vitu vyenye thamani zaidi ya...

Nyumba ya Roberto Firmino yavamiwa na kuibiwa vitu vyenye thamani zaidi ya milioni 180.

495
0
SHARE

firl

Hii ni majanga juu ya majanga, wakati akiwa kwenye shtaka lake la kuendesha gari akiwa amelewa tatizo lingine limemtokea Roberto Filmino ambapo nyumba yake imevamiwa na kuibiwa vitu vyenye thamani zaidi ya Tsh 180,000,000.

Taarifa ya polisi inasema kwamba wezi hao walikua wamevaa nguo za kufunika kichwa walivamia nyumba ya mchezaji huyo mwenye miaka 25 na kuiba vito vya thamani kama saa, cheni na nguo zenye jumla ya Tsh milioni 180.

Hili sio tukio la kwanza kwa Firmino kutokea, December 22 Firmino na mke wake na watoto wake wadogo wawili walihamishiwa kwenye hotel baada ya tukio hilo kutokea tatizo kama hili lakini hakuna madhara yaliyokea wala upotevu wa mali.

Polisi wa Merseyside wametoa taarifa kwamba wanafanya uchunguzi wao kutokana na historia ya kufatwa sana na wezi. Kwanini nyumba yao inamekua target ya wezi kiasi hiki.

Wanye Rooney alinusurika kuibiwa wakati anacheza mechi testimonial lakini polisi waliwahi eneo la tukio. Romelu Lukaku aliibiwa wakati yupo kwenye mechi za kufuzu michuano ya Euro 2016. Matukio ya wizi kwenye nyumba za wanamichezo yamekua mengi sana.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here