Home Ligi EPL Mesut Ozil ; “Wenger akiendelea na mimi nabaki”

Mesut Ozil ; “Wenger akiendelea na mimi nabaki”

1519
0
SHARE

ozill

Wachezaji nyota Mesut Ozil na Alexis Sanchez wamebakiwa na miezi 18 tu hadi mikataba yao ya sasa iishe. Hivyo basi ni salama kwa club ya Arsenal kuwapa mikataba mipya kwa sasa hivi kaba miakataba yao haijaisha.

Kumetoka story nyingi sana kuhusu wachezaji hawa na jinsi watakavyo saini mikataba yao mipya. Kwa upande wa Sanchez imeripotiwa kwamba wakikubaliana swala zima la mshahara wake basi ataweza kusaini mkataba mpya.

Upande wa Ozil aliwahi kusema, “Nina furaha sana hapa Arsenal na ningependa kusema kwamba nipo tayari kusaini mkataba mpya. Mashabiki wanataka nibaki basi nitabaki hapa.”.

Ozil aliongeza,“Club inajua kwamba nipo hapa kwasababu ya Arsene Wenger. Yeye ndiye aliyesajili hapa na ndiye ananiamini. Nataka kuwa muwazi kwamba atakacho kifanya meneja kina ushawishi kwangu”.

Kuweka vizuri kuhusu kauli ya Ozil ni kwamba angependa kuna Wenger anaendelea kuwa kocha wa Arsenal ili aendelee kumuamini kwenye kikosi chao kama anavyomuamini sasa hivi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here