Home Kitaifa Timu pekee ya Zanzibar iliyofuzu nusu fainali inakutana na mziki wa Azam

Timu pekee ya Zanzibar iliyofuzu nusu fainali inakutana na mziki wa Azam

883
0
SHARE

dsc_0321

Taifa Jang’ombe ndio timu pekee kutoka Zanzibar ambayo imefuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2017.

Taifa imefuzu baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya URA ya Uganda ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wa taji hilo. Bao la Mohamed Said ‘Messi wa Unguja’ limeifanya Taifa ifikishe pointi tisa pointi moja nyuma ya Simba ambao ni vinara wa Kundi A.

dsc_0322

Taifa Jang’ombe imefuzu ikizipiku timu nyingine za Zanzibar kama KVZ na mahasimu wao Jang’ombe Boys.

Watacheza nusu fainali ya kwanza saa 10:15 jioni Jumanne January 10 dhidi ya Azam ambao ndio vinara wa Kundi A.

dsc_0332

Taifa Jang’ombe imeungana na iimu nyingine zilizofuzu hatua ya nusu fainali ni pamoja na Azam, Yanga na Simba ambazo zote zinatoka Tanzania bara.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here