Home Kitaifa Kipigo kutoka Azam ni darasa tosha – Mwambusi

Kipigo kutoka Azam ni darasa tosha – Mwambusi

836
0
SHARE

dsc_0514

Kipigo cha mabao 4-0 walichotoa Azam kwa Yanga kimegeuka darasa tosha kwa upabde wa Yanga kwamba hawatakiwi kudharau mechi hata kama wamefuzu kwa hatua nyingine inayofata.

“Wachezaji wetu walicheza huku kichwani wakijua tumesha vuka kwa hiyo hakukuwa na haja ya kuweka nguvu zaidi lakini hiki kitu ni somo kwetu kwamba tunatakiwa tucheze mechi zetu kwa uangalifu mkubwa kwa sababu tumepoteza hii mechi tunakubali matokeo,” amesema kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi muda mfupi baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Azam.

“Tuli-relax mno hakuna juhudi yoyote iliyofanyika uwanjani mchezaji mmoja-mmoja, tuliacha njia wazi wenzetu wakacheza kwa nguvu zao zote na kuweza kupata goli nne na kwetu ni masikitiko kwa sababu tumepoteza mechi lakini tutarekebisha makosa yetu.”

Tangu Yanga ikumbane na kipigo kikali cha magoli 5-0 kutoka kwa Simba, ilikuwa haijafungwa kwa muda mrefu magoli zaidi ya matatu. Mwaka 2012 Simba iliifunga Yanga magoli 5-0 kwenye uwanja wa taifa hadi leo ambapo usikuwa January 7, 2017 Azam ikataka kurudia historia ya Simba kwenye michuano ya Mapinduzi Cup.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here