Home Kitaifa Hakuna tunachotaka kwa Yanga zaidi ya Matokeo – Mayanja

Hakuna tunachotaka kwa Yanga zaidi ya Matokeo – Mayanja

884
0
SHARE

20170108_211159

Kocha msaidizi wa timu ya Simba Jackson Mayanja amesema hakuna kitu kingine wanachohitaji kwenye mechi yao ya nusu fainali zaidi ya matokeo ya ushindi. Jumanne January 10, 2017 Simba itacheza mechi ya nusu fainali ya Mapinduzi Cup dhidi ya Yanga ambao ni wapinzani wao wakuu wa soka la Tanzania.

“Sisi tumekuja kupata matokeo kama ikitokea tukakosa matokeo itakuwa ni bahati mbaya lakini tunataka sana matokeo,” anasema Mayanja baada ya ushindi wa Simba 2-0 Jang’ombe Boys.

Kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Kagera Sugar na Coastal Union amesema mechi itakuwa nzuri kwa sababu mshindi wa mechi hiyo atafuzu kucheza fainali ya kombe la Mapinduzi 2017.

“Mechi itakuwa nzuri sana watu waje kwa wingi waitazame kwa sababu mmoja wetu kati ya Simba au Yanga atakaeshinda anakwenda fainali.”

Kuhusu mechi yao dhidi ya Jang’ombe Boys kukamilisha hatua ya makundi, Mayanja amesema : “Game ilikuwa nzuri, tumefanya vizuri tumepata magoli mawili na tunaelekea kwenye hatua ya nusu fainali.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here