Home Kimataifa Video: Samatta alivyozipokea taarifa za kuondoka kwa Ndidi

Video: Samatta alivyozipokea taarifa za kuondoka kwa Ndidi

2280
0
SHARE

ndindi

Baada ya kiungo wa KRC Genk Wilfred Ndidi kujiunga na klabu ya Leicester City inayoshiriki ligi kuu ya England, Mbwana Samatta ambaye walikuwa wanacheza timu mmoja na Ndindi ameelezea namna alivyozipokea taarifa za kuondoka kwa Ndindi.

Ndidi ambaye ni raia wa Nigeria anacheza nafasi ya kiungo wa ulinzi na anatajwa kwenda kuziba nafasi ya Ng’olo Kante aliyesajiliwa na Chelsea msimu huu.

Tayari nyota huyo ameshasaini mkataba wa miaka mitano na nusu kuitumikkia Leicester kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 15 huenda akajumuishwa kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wa FA Cup dhidi ya Everton.

Mtangazaji wa BBC Salim Kikeke amepost video ya kipindi cha Dira ya Dunia kwenye ukurasa wake wa Instagram namna ambavyo Samatta alivyopokea habari za kuondoka kwa Ndidi kwenye klabu ya Genk.

Samatta amzungumzia Ndidi

A video posted by Salim Kikeke (@salim_kikeke) on

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here