Home Kitaifa Watoza ushuru wa Uganda wameikwamisha Simba kufikisha pointi 9 Mapinduzi Cup

Watoza ushuru wa Uganda wameikwamisha Simba kufikisha pointi 9 Mapinduzi Cup

757
0
SHARE

dsc_0795

Simba imeshindwa kupata ushindi dhidi ya URA ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa tatu wa Kundi A usiku saa wa January 5.

 

Licha ya sare hiyo Simba bado inaongoza Kundi A ikiwa na pointi saba pointi moja mbele ya Jang’ombe Boys yenye pointi sita (timu zote zimeshacheza mechi tatu).

dsc_0739

Manyika Jr na Laudit Mavugo walianza kwenye kikosi cha kwanza tofauti na siku za karibuni ambapo mara nyingi Mavugo amekuwa akiingia kutoka benchi wakati Manyika Jr yeye hakupata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu.

dsc_0695

Mchezo wa mapema uliishihudia Jang’ombe Boys ikipata ushindi mnono wa magoli 3-1 dhidi ya KVZ timu ambayo bado haijapata pointi hadi sasa.

dsc_0672

Simba itacheza mechi yake ya mwisho ya hatua ya makundi kwa kukipiga dhidi ya Jang’ombe Boys ambayo inatumikiwa na Abdi Kassim Babi kiungo wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania.

dsc_0697

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here