Home Kitaifa Mfungaji wa hat-trick ya kwanza Mapinduzi anaisubiri Simba

Mfungaji wa hat-trick ya kwanza Mapinduzi anaisubiri Simba

880
0
SHARE

dsc_0659

Abdi-samad Kassim Ali ni mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwenye mashindano ya 11 ya Mapinduzi 2017, wakati Jang’ombe Boys ikipata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya KVZ.

Simba itacheza dhidi ya Jang’ombe Boys siku ya Jumapili Janury 8 lakini mchezaji huyo amesema siku hiyo lazima Simba ipotee.

“Naahidi mnyama atapotea ili kuhakikisha tunamaliza mashindano hayo salama, najiamini kwa sababu kila kitu kinawezekana tunafanya mazoezi tukishirikiana na wachezaji wenzangu tukaweka maelekezo ya mwalimu uwanjani tutafanikiwa,” anasema mchezaji huyo aliyefunga magoli yote matatu ndani ya kipindi cha kwanza.

“Ni hat-trick yangu ya kwanza kwenye maisha yangu ya soka. Siri ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo ni mazoezi na kufata maelekezon ya kocha hakuna jambo jingine zaidi.”

Abdi-samad amemfikia Labama Bogota wote wakiwa na magoli matatu nyuma ya Simon Msuva mwenye magoli manne akiongoza orodha ya wafungaji kwenye michuano ya Mapinduzi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here