Home Kitaifa Babi bado yupoyupo sana…

Babi bado yupoyupo sana…

650
0
SHARE

20170104_095102

Kama ulikuwa na mawazo kwamba Abdi Kasim Babi astaafu soka basi umechemka, jamaa bado yupoyupo kwenye sana kwenye soka, hii ni baada ya kueleza mipango yake mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Jang’ombe Boys vs URA ambapo Jang’ombe Boys walipata ushindi wa magoli 2-1.

Kwa namna ambavyo mkongwe huyo wa klabu ya Yanga, Azam na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ alivyoefunguka kuhusu mipango yake ya baadae kwenye soka, inadhihirisha bado yupoyupo sana kwenye game.

Mipango ya kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania

Mara ya mwisho kufanya mahojiano na Babi ilikuwa January 2016 ambapo alieleza mipango yake ya kurudi nje kucheza soka la kulipwa alikokuwa akicheza (Malaysia) kabla ya kurejea Zanzibar.

“Nipo katika kutafuta zaidi, nafasi bado zipo kwa hiyo nipo hapa kwa likizo ndio maana nacheza ligi kwa sababu ya kupandisha kiwango changu na watu waone. Mimi nafurahi kucheza soka.”

Taifa Jang’ombe kwenda Jang’ombe Boys

“Taifa Jang’ombe na Jang’ombe Boys ni zenye upinzani mkubwa sana hapa visiwani Zanzibar ni kama Simba na Yanga kwa upande wa Dar. Babi alikuwa Taifa Jang’ombe lakini amehama na kujiunga na Jang’ombe Boys kitu ambacho kimepokelewa kwa furaha kwa upande wa Jang’ombe Boys huku Babi akionekana ni msaliti kwa Taifa Jang’ombe.”

“Kwa upande wangu mimi ni kawaida, watu wakumbuke nimetoka wapi nilikuwa Yanga, hii ni soka kutoka Taifa Jang’ombe kwenda Jang’ombe Boys bado ni nyumbani. Kulikuwa na matatizo kidogo (Taifa Jang’ombe) sasa kwa sababu mimi ni mchezaji mzoefu, sikutaka kuharibu CV yangu ndiyo maana nikaondoka na kuja sehemu yenye nidhamu timu ambayo itaniheshimu na tukafanya kazi.”

Kuelekea mchezo wa Jang’ombe Boys vs Simba

Jang’ombe Boys bado ina michezo miwili katika Kundi A, moja kati ya mechi hizo ni dhidi ya Simba ambao ni vinara wa kundi hilo wakiwa na pointi 6 baada ya mechi 2. Babi anaifaham vizuri Simba kwa sababu amekutana nayo mara nyingi wakati akicheza Yanga na ligi kuu Tanzania bara.

“Ni mchezo wa kawaida, cha msingi ni kuwahamasisha wachezaji wenzangu kujiamini kwa sababu na mimi mwenyewe nitakuwepo uwanjani tutacheza kitimu zaidi ili kupata ushindi. Sisi hatujali, timu yoyote tutacheza nayo iwe Simba, Yanga au Azam tupo tayari kwa mechi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here