Home Kitaifa Ushindi wa Simba vs KVZ ulivyobeba maana ya January 3 kwa Mzamiru

Ushindi wa Simba vs KVZ ulivyobeba maana ya January 3 kwa Mzamiru

1127
0
SHARE

dsc_0194

Kama ulikua hujui, leo January 3 ilikuwa ni birthday ya Muzamiru Yassin kiungo anayefanya vizuri kwa sasa kwenye klabu ya Simba na ligi kuu Tanzania bara kutokana na kiwango kizuri anachokionesha uwanjani.

Wakati anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa, Simba ilikuwa ina ratiba ya kucheza mechi ya mapinduzi Cup dhidi ya KVZ.

Mzamiru amesema siku ya leo muda mwingi alikuwa akiomba kwa Mungu aisaidie timu yake kupata ushindi na imetokea hivyo huku goli la ushindi akifunga yeye mwenyewe. Mzamiru amesema hatoisahau birthday yake ya mwaka huu kwa sababu amefanikiwa kufunga goli lililoipa Simba ushindi muhimu kwenye michuano ya Mapinduzi.

“Nilikua namuomba sana Mwenyezi Mungu siku yangu ya kuzaliwa niipatie timu yangu ushindi na nashukuru imetokea kama nilivyooma,” anasema Mzamiru ambaye alisajiliwa na Simba kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Kama kawaida, birthday za siku hizi kuogeshwa ni imekuwa ni desturi. Wachezaji wa wenzake wa Simba walimuogesha kama ku-show love kwa mshkaji wao.

“Nimeongeshwa sana matope, juice bila kusahau maji.”

Jambo la kuvutia ni kwamba, Mzamiru ndiye aliyefunga goli pekee la Simba lililoipa ushindi wa goli 1-0.

“Birthday zangu huwa siziandai kwa sababu mara nyingi huwa nakuwa kwenye mashindanio, mwaka jana pia nilikuwa kwenye mashindano haya (Mapinduzi Cup) wakati bado nipo Mtibwa. Lakini hii nitraikumbuka sana kwa sababu nimeisaidia timu yangu kupata ushndi na kama tungepoteza mechi hii ningesikitika sana.”

“Sasa hivi napata nafasi ya kufunga kwa sababu nacheza nyuma ya mshambuliaji mmoja.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here