Home Kitaifa Mwambusi ametoa 5 kwa Msuva

Mwambusi ametoa 5 kwa Msuva

1413
0
SHARE

20170103_110206

Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema, amempa tano kiungo mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva lakini akasisitiza kuwa mchezaji huyo wa Taifa Stars ni bora zaidi ya alivyo sasa.

Msuva alifunga magoli mawili kwenye ushindi wa 6-0 dhidi ya Jamhuri katika michuano ya Mapinduzi Cup huku akisaidia kupatikana kwa magoli mangine yaliyofungwa na Donald Ngoma.

“Amejitahidi Simon (Msuva) lakini bado tunahitaji afanye zaidi ya hapo, tumeshakaa na mwalimu tumemuelekeza kwa sababu bado anamakosa madogomadogo anahitaji kuyarekebisha na sisi tunaendanae tunaonesha nuru mbele yake, Simon ni mzuri sana kuliko hivi tunavyomuona,” anasema Mwambusi baada ya mchezo wao dhidi ya Jamhuri.

“Msuva amekuwa na mchango mkubwa sana kwa sababu nusu ya magoli yote ya Yanga yametoka kwake. Ni mchezaji mwandamizi ndani ya Yanga muhimu kama wachezaji wengine lakini tunataka aongeze zaidi bidii ili kufika pale tunapopategemea.”

Msuva amekuwa mtamu tangu kwenye VPL na anachokifanya sasa kwenye Mapinduzi Cup ni mwendelezo wa kile alichokuwa akikifanya kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara.

Kama unakumbuka vizuri, Msuva aliwahi kuwa mchezaji bora wa VPL huku akishinda pia tuzo ya ufungaji bora wa VPL ndani ya msimu mmoja (2014-15).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here